Wednesday, November 29, 2017

CCM yatwaa kata tatu udiwani, Mnadani Nasibu, Mndeme

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.

MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro , Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha wananchi kwenye kata husika.

Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.

“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya madiwani wa kata husika kujiuzulu”

“Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao  ambapo zoezi hilo limekamilika bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya  kampeni hadi siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”

Amesema, katika uchaguzi huo jumla ya vyama vitano vilishiriki kwa kusimamisha wagombea wao kuomba ridhaa kwa wananchi ambavyo vilikuwa ni CCM, CHADEMA, ACT- Wazalendo, CUF na NCCR Mageuzi.

Vyeti hivyo vilikabidhiwa kwa Salehe Msengesi (CCM) ambaye alishinda nafasi ya udiwani katika kata ya Weruweru, Martini Munis (CCM) wa kata ya Machame Magharibi na Nasibu Mndeme (CCM) kata ya Mnadani.

Naye diwani mteule wa kata ya Weruweru, Salehe Msingesi  alisema  ahadi alizozitoa kwenye mikutano yake ya kampeni atahakikisha kuwa zinatekelezwa kwa uhakika ikiwemo kutatuankero ya barabara ambazo kwenye hiyo kata hazipitiki msimu mzima wa mwaka kutokana na uharibifu wake.

Kwa upande wake diwani mteule wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme
Akizungumzia utekelezaji wa ahadi alizotoa  diwani mteule wa kata ya Machame Magharibi , Martini Munisi alisema ahadi alizotoa atasimamia ili ziweze kufanikiwa kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri pamoja na Chama chake ili kuweza kusogeza huduma kwa jamii kwa wakati.

“Natambua kuwa katika kata niliyochaguliwa kuna changamoto nyingi sana ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara  , shule zote za msingi  zilizoko kwenye kata zinahitaji ukarabati wa majengo haswa shule ya Msingi Kyeri ambayo jiko lake limeanguka na linahitaji ukarabati wa haraka  ”alisema.

Tuesday, November 28, 2017

Shirika la Kivulini lasaidia uanzishaji Kiwanda Shule ya Wasichana Bwiru

Uzinduzi wa kiwanda kidogo katika shule ya wasichana ya kidato cha tano na sita Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akikagua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa shuleni hapo.

Mgeni rasmi akijionea picha mbalimbali zinazochorwa shuleni hapo.

Mgeni rasmi akijionea utengenezaji wa sabuni pamoja na dawa za chooni.

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mkuu wa shule ya wasichana Bwiru, Mwalimu Mackrida Shija akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga akizungumza kwenye ufunguzi huo ambapo aliahidi ushirikiano katika kuendeleza kiwanda hicho.

Mwanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru, Dorophy James (kushoto), akisoma risala ya ufunguzi. Kulia pia ni mwanafunzi wa shule hiyo Delvina Mollel.

Wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally kwenye uzinduzi huo.

Viongozi mbalimbali.

Maafisa wa ulinzi.

Wanafuzni wa shule ya wasichana Bwiru wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.

Wanafunzi wakimkabidhi zawadi mgeni rasmi.

Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.

Wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na Afisa Elimu Sekondari wilayani Ilemela.

Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.

Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.

Burudani kutoka kwa kikundi cha ngoma asilia, Chapa Kazi kutoka Nyamadoke wilayani Ilemela.

Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI.

Karibu shule ya Wasichana Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza ili kujifunza kuhusu uanzishwaji wa Viwanda.

KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION YAWAKUTANISHA MADALALI WA BIMA, WARUDISHA SHUKURANI KATIKA JAMII.

Mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma ambaye ni Meneja Mkazi wa Africa Practice mshauri  akitoa shukurani zake za dhati kwa Kampuni ya Bima ya Resolution kwa kuwakutanisha Madalali wa Bima 'Insurance Brokers' toka sehemu tofauti nchini ambapo kwa kufanya hivyo itaongeza zaidi ufanisi na ushirikiano baina yao na Kampuni ya Bima ya Resolution.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mambo mbalimbali kuhusiana na kampuni hiyo na kuwashukuru madalali wa Bima kwa kwa kuungana nao katika chakula cha usiku, pamoja na hayo alisema kuwa wapo Kenya, Uganda na Tanzania, kwa Tanzania wapo Dar es salaam na Arusha lakini hivi karibuni watafika Zanzibar na Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo akieleza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo la kurudisha shukurani, ambapo pia alizitaja baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa nipamoja na; Travel Plan, Medical plan, Liability plan,Home Insurance,Marine insurance na Motor Private Insurance.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya  Resolution  Tanzania Bi. Maryanne Mugo (aliye simama nyuma) akiwatambulisha viongozi wa Idara mbalimbali katika kampuni ya Bima ya Resolution wa nchini Tanzania.

Bwana Melkizedech Nyau ambaye ni mtakwimu wa Bima kutoka kampuni ya Bima ya Resolution akielezea bima ya Afya Bora kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini kuanzia mwaka 0 hadi 64 ambao ni kama Bodaboda, Mama ntilie,wauza maandazi pamoja na makundi mbalimbali yanayofanana na hayo. Alieleza kuwa ili kujiunga na Bima hiyo itakuwa vizuri watu wawe katika kundi au Vikoba waweze kupata kwa pamoja huduma hiyo bora kutoka kampuni ya Resolution.

Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku ambaye pia ni Mchekeshaji maarufu hapa Nchini Tanzania akiendelea kutoa taratibu mbalimbali wakati wa  chakula cha usiku kilicho andaliwa na Shirika la Bima la Resulution katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.


Muwezeshaji wa hafra hiyo Bw. Evance Bukuku akiwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na bima.

Bi. Mailda William(Kushoto) kutoka Aste Insurance Brokers ambao walishinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Msichana ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.


Bi. Jenifa Projest (Kulia) kutoka Aste Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni Rasmi Bw. Charles Washoma baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Salvation Army  ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.

 Bi. Fauzia Bairu (Kushoto) kutoka Pioneer Insurance Brokers akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati baada ya  kushinda katika bahati nasibu kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution ambapo kiasi cha fedha Tsh 500,000 zitaenda kwa asasi ya kiraia ya Sustainable Education ikiwa ni kurudisha Shukurani kwa jamii kutoka kampuni ya bima ya Resolution.

 Bw. Emmanuel Mkindi, Meneja wa Maendeleo ya Biashara- Biashara kwa ujumla kutoka Kampuni ya Bima ya Resolution akitoa neno la shukurani kwa madalali wote wa bima waliofika katika tukio lao la 'Appreciation Dinner' ambapo kaulimbiu yao inasema 'Protecting what you value' yani tunalinda unachokithamini.

Madalali wa Bima wakiwa katika hafra ya chakula cha usiku iliyo andaliwa na Kampuni ya Bima ya Resolution kwa ajili ya kurudisha shukurani kwa jamii.

Monday, November 27, 2017

Wakaazi wa Arusha watambulishwa bidhaa bora za umeme jua

Mkazi wa Arusha Mzava Nsanjiwa akitazama jiko linalotumia nishati ya jua katika banda la Kampuni ya Sola ya Sunking katika maonyesho yaliyofanyika kwa ajili ya kuhamasisha wakaazi wa Arusha kutumia bidhaa za sola zilizo bora, katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha. Picha na Mpigapicha wetu.

Mkazi wa Jiji la Arusha Yohana (watatu kulia) akitazama bidhaa mbalimbali za majumbani zinazotumia nishati ya jua katika mabanda ya kampuni ya solar ya Sunking, katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha. Picha na Mpigapicha wetu.


Mkazi wa Jiji la Arusha Yohana (watatu kulia) akitazama bidhaa mbalimbali za majumbani zinazotumia nishati ya jua katika mabanda ya kampuni ya solar Sister, katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha. Picha na Mpigapicha wetu.

Mkazi wa Arusha Bi. Dora Mkini akitazama jiko linalotumia nishati ya jua kutoka katika kampuni ya Sunking katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kilombero jijini Arusha. Picha na Mpigapicha wetu.

Sunday, November 26, 2017

Naibu Waziri Mavunde agawa mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbali kutoka kampuni ya HiTECH International kwa vikundi 31 katika jimbo lake la Dodoma Mjini. Mashine alizozitoa Naibu Waziri ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga (incubators- mayai 1056 na mayai 528) mashine za matofali (umeme na manual), mashine za Popcorn zenye matairi, vyerehani, mashine za kutengeneza chaki (chaki 50,000-80,000 kwa siku), mashine za kunyonyolea kuku mpaka kuku 500 kwa siku. Mavunde ametoa mashine hizo zenye thamani ya milioni 55.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika uchaguzi wa mwaka 2015 kuwezesha wananchi ili wajikomboe kiuchumi lakini pia kuunga mkono mpango wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa vikundi mbalimbali vya Dodoma Mjini. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kukabidhi mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini.

Friday, November 24, 2017

DR SHIKA NI NOMA, AHAIDI BILIONI 2 KWA WENYE NJAA YA ELIMU

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu leo amezidua rasmi chuo cha Sayansi ya afya kilichopo Mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo uzinduzi huo umeambatana na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo hicho. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Kahama akiwemo Mtanzania aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Dr. Louis Shika ambaye ameahidi kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki dunia.

Wednesday, November 22, 2017

Serikali kulala mbele na wanaokiuka bei elekezi ya mbolea

Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Tawala na Washauri wa kilimo wa Mkoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Katika KUKUMBI WA kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya Nov 21 ,2017.


Na Emanuel Madafa, Mbeya


SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa  wakati akifungua  mkutano wamakatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .

Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara  itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara yake

Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala  wanaouza kwa bei elekezi ya serikali  hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .

Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na Geita wapo wafanyabiashara  ambao  sio waaminifu wamekuwa wakifungua  mifuko na kuuza mbolea ya kupandia  (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi  laki moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50  badala ya bei elekezi ya shilingi  elfu hamisini na moja.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima  hasa katika kipindi cha mavuno.

Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara  kote nchini kuacha tabia hiyo  mara moja ili kumpa fursa Wakala aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .

Mkutano huo unalenga  kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu  mifumo mipya iliyoanzishwa  ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei  nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye tija.

Mwisho.




Washiriki  wa Mkutano wa Makatibu Tawala Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaolenga  kuongeza uwezo uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System -BPS) na Usimamizi wa bei ya mbolea ,katika ukumbu wa mikutano Mkapa jijini Mbeya Nov 21 mwaka huu.

Mshiriki akichangia katika Mkutano huo........

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...