Monday, October 5, 2015

MANGUNGU AZINDUA RASMI KAMPENI ZA UBUNGE MBAGALA

  Mgombea ubunge  jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule. (Na Mpigapicha Wetu)
  Mgombea ubunge  jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule. 
 Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Chamazi Shule.
Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea wa ubunge wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu.
 Mgombea wa Ubunge  katika jimbo la Mbagala  kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu (kushoto) akitambulisha wagombea wa udiwani  wa kata za jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.
 Wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano huo.
 Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu, Yusuf Manji akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa ubunge wa jimbo la Mbagala  kwa tiketi ya CCM, Issa Mangungu kwenye uzinduzi wa mikutano ya kampeni zake.

Na Mwandishi Wetu



MGOMBEA wa Ubunge wa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo jipya  la Mbagala Issa Mangungu, amesema endapo atachaguliwa  kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha vijana wanapewa  kipaumbele katika kupata ajira.


Mangungu aliyasema hayo juzi wakati wa uzinduzi rasm wa kampeni zake katika jimbo hilo, zilizofanyika kwenye viwanja vya 
Chamazi Shule Jijini Dar es Salaam, kuwa atahakikisha suala la ufundi kwa vijana linapewa kipaumbele.
 Alisema katika kuhakikisha vijana wanapata ajira ataishawishi Serikali kufungua tawi la Chuo cha Ufundi (VETA), katika Jimbo hilo ili vijana waweze kusoma na kupata 

kazi. "Nitahakikisha napigania uanzishwaji wa tawi la Veta katika la Mbagala hili vijana waweze kupata mafunzo ya ajira"alisema Mangungu. Katika hatua nyingine Mangungu alisema kuna tatizo la shule katika baadhi ya kata atahakikisha wanajenga shule ili kuepusha wanafunzi kutembea kwa muda mrefu kupata elimu.

Alisema kuna tatizo la kutokuwa na Shule za Sekondari haswa za kuanzia kidato cha tano, hivyo watajipanga kuongeza madarasa na kujenda shule nyingine za Sekondari."Kwenye sehemu ya shule za Sekondari tutaongeza majengo ya madarasa ili wanafunzi wakaofanya vizuri wapate nafasi ya kuendelea na kuna kata nyingine tutajenga shule za Sekondari"alisema Mangungu.

Alisema kuwa katika upande mwingine atahakikisha madereva wa bodaboda wanatambulika kwa sababu nao ni wapo kwenye ajira.Mangungu alisema kuwa lazima madereva wa bodaboda wawe kwenye ajira rasmi, hivyo kama mbunge atawatetea madereva hao.

Alisema kuna tatizo la Maji na Barabara vipi ndani ya vipaumbele vyake ana amini akipata nafasi  yeye na madiwani wake wa CCM watafavifanyia kazi.

Mangungu amewataka wakazi wa mbagala kumchagua yeye katika nafasi ya ubunge, ikiwa pamoja na kumchagua mgombea wa Urais 

John Magufuli na kuchagua madiwani wa CCM, ili waweze kuwa kitu kimoja na kuweza kushirikiana katika kuwaletea maendeo.

Katika mkutano huo wa ufunguzi wa Kampeni ya za mbunge huyo, mgeni rasmi alikuwa Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC), ambaye aliwataka wakazi wa jimbo hilo wasifanye makosa kumchagua mbunge wa upinzani. 

Nahodha alisema ana amini wakimchagua mbunge, Rais na madiwani wa CCM wataweza kufanikisha ahadi zao.

Alisema CCM ina ilani nzuri inayotekelezeka kwa wananchi wake hivyo kuna kila sababu ya kulitambua hilo.

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, amewataka wananchi wa jimbo hilo kutofanya makosa ya kuwapata uongozi wa wa vyama vya upinzani, kwa sababu hawana sera, hivyo watumie nafasi hiyo kuchagua wagombea wa CCM.

Madabida alisema kuwa siku ya Oktoba 25, wahakikishe wanajitokeza kwa wingi kwenda kuwapiga kura na kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika mkutano huo mgombea Ubunge aliwatambulisha wagombea Udiwani wake katika Kata 10 zilizopo katika Jimbo hilo akiwemo Yusuph Manji na Said Fella.


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...