Thursday, October 1, 2015

Mama Samia Suluhu Azulu Kaburi la Baba wa Taifa Butiama

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa nyumbani kwake Kijijini Mwitongo, kulia ni Mkuu wa Wilaya Butiama, Annarose Nyamubi akimsaidia.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa nyumbani kwake Kijijini Mwitongo, kulia ni Mkuu wa Wilaya Butiama, Annarose Nyamubi akimsaidia.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kaburi la Baba wa Taifa.
Kiongozi wa Ukoo na familia ya Baba wa Taifa, Chifu Japhet Wanzagi Nyerere (kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka kwa wanafamilia mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan leo amezulu kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na kuisalimu familia ya baba wa taifa kijijini kwake Mwitongo katika Kata ya Butiama.

Mama Suluhu Hassan ametembelea kaburi hilo akiwa na msafara wake wa kampeni pamoja na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa ikiwa ni ishara ya heshima alipokuwa katika ziara yake ya kampeni Mjini Musoma kuinadi ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Bi. Suluhu Hassan amepokelewa na Kiongozi wa Ukoo na familia ya Baba wa Taifa, Chifu Japhet Wanzagi Nyerere ambaye alisema amefarijika kuona CCM na viongozi wake bado wanamkumbuka Baba wa Taifa na kutambua mchango wake. Chifu Wanzagi akizungumza alimuombea, Bi. Suluhu Hassan kila heri katika kuomba ridhaa ya Watanzania kuiongoza tena nchini.

Kwa upande wake Bi. Suluhu Hassan akizungumza mbali na kuishukuru famili ya Baba wa Taifa kwa mapokezi alisema bado wanaimani kuwa nyumbani kwa Baba wa Taifa ni kitovu cha Chama Cha Mapinduzi hivyo wataendelea kumuenzi na kutambua mchango wake mkubwa kwa chama na taifa kwa jumla. Bi. Suluhu Hassan pia aliweka shada la maua kwenye kaburi hilo pamoja na kupewa zawadi na familia ya baba wa taifa. 

Bi. Samia Hassan leo ameendelea na ziara yake kwa kuuanza Mkoa wa Simiyu akitumia barabara huku akiwasalimu wananchi njiani na kufanya mikutano ya hadhara majimbo kadhaa ya mkoa huo.

Kiongozi wa Ukoo na familia ya Baba wa Taifa, Chifu Japhet Wanzagi Nyerere (kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka kwa wanafamilia mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kulia), akiwa nyumbani kwa baba wa taifa pamoja na familia ya baba wa taifa na viongozi alioambatana nao.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati), akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa baba wa taifa pamoja na familia ya baba wa taifa na viongozi alioambatana nao.
Mkuu wa Wilaya Butiama, Annarose Nyamubi (wa kwanza kushoto) akimkaribisha mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu nyumbani kwa baba wa taifa.
Kiongozi wa Ukoo na familia ya Baba wa Taifa, Chifu Japhet Wanzagi Nyerere (kushoto) akimkaribisha mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan nyumbani kwa baba wa taifa.
Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwashukuru wanafamilia kwa mapokezi.
Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akielekea eneo lilipo kaburi la Baba wa Taifa tayari kutoa heshima alipotembelea eneo hilo leo wilayani Butiama.
Kushoto ni sheikh akiomba dua mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati Bi. Samia Suluhu Hassan alipotembelea na msafara wake. 
Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa madhehebu ya kikristu akiomba mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati Bi. Samia Suluhu Hassan alipotembelea pamoja na msafara wake. 
 Msafara Msafara wa magari ya mgombea mwenza wa CCM ukiwa nyumbani kwa baba wa taifa.
Msafara wa magari ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan ukiwa nyiani kuelekea Mkoani Simiyu mara baada ya kuzulu kaburi la baba wa taifa.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...