Monday, October 5, 2015

MAMA SHUJAA WA CHAKULA YAWAPELEKA WATATU NJE YA NCHI

Codes
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2014 Linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow Bahati Muriga(Kulia)   yenye kauli mbiu kuwa Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake Inalipa, akielezea kwa undani juu ya Safari yake ya Kwenda Marekani pia Kushukuru Oxfam kwa kupata nafasi hiyo
Aliyekuwa Mshiriki wa Shidano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Eva Mogeni (Kushoto) akielezea kuhusu safari yao ya kwenda Addis Ababa Ethiopia kwa ajili ya  kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA) na kutunga Sera juu ya kilimo na kupaza sauti za wakulima wadogo hasa wanawake ili kupata Fursa sawa katika Kilimo.
Edna Kiogwe  aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akielezea jambo kuhusiana na  kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA) utakaofanyika Adis Ababa nchini Ethiophia Oktoba 11hadi 15 mwaka huu.
Waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula akiwemo Mshindi wa Shindano hilo kwa Mwaka 2014 Msimu wa tatu Bahati Muriga Wamepokea Mwaliko wa Kwenda Washington DC Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa Siku ya Chakula duniani unaotarajiwa kufanyika Washington DC  na Addis Ababa kwa ajili ya Kuhudhuria Mikutano Mbalimbali. Kati ya hao Bahati Muriga atakwenda Marekani na Edina  Kiogwe pamoja na Eva Mogeniw watakwenda  kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA)


Eluka Kibona ambaye ni Meneja wa Utetezi wa Oxfam Tanzania alisema kuwa Bahati Muliga atahudhuria mikutano mbalimbali nchini humo inayohusu masuala ya Chakula na Kilimo wakati wa wiki zote Mbili atakazokuwa huko. Aliongeza kuwa Oxfam imethibitisha kupokea Barua ya Mwaliko wa Muriga na atahudhulia kikamilifu makongamano hayo ili apate kujifunza na kupata ujuzi ambao atautumia kwa kuwashirikisha wakulima wanawake wadogo wadogo.


 “Muriga anakwenda kuhudhuria mikutano mingi, ambayo itafanyika Washington DC na Ohio. Hii ni fursa adimu ambayo Shirika la Oxfam kupitia Oxfam Tanzania limeamua kutoa kwa kinamama hawa ili wajifunze zaidi kilimo cha kisasa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Eluka.

Wakati huo huo Oxfam wakishirikiana na Shirika la Kimataifa la Action Aid na African Union Commission limetoa Mwaliko kwa washiriki wawili kati ya walioshiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne ambao ni  Edina Kiogwe na Eva Mogeni kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA) utakaofanyika Adis Ababa nchini Ethiophia unaotarajiwa kuanza Tarehe 11 Octoba mwaka huu

Eluka alisema Mkutano huo unawakutanisha na kuwaleta pamoja vikundi vya wazalishaji chakula wadogo kutoka sehemu mbalimbali Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wao wanavyohusika na watengeneza sera na kutoa mchango wa pamoja kukabiliana na mahitaji yao.

Akizungumzia safari hiyo Mshindi wa Mama Shuja wa Chakula Msimu wa Tatu Bahati Muriga alisema hiyo ni fursa mpya kwake na anajua kwa kuhudhuria mkutano huo atapata maoni mapya kuhusiana na sera ya kilimo, uwekezaji katika miradi, lakini kubwa zaidi ni kwake ni mbinu mbadala za kilimo cha kisasa sambamba na kushuhudia nini wengine wanafanya katika kilimo.

 “Nitapata maoni mapya ninakwenda kwa niaba ya wakulima wadogowadogo Tanzania, lakini kuongeza ujuzi na kupata mikakati mbalimbali kuhusu kilimo, kujuana na kubadilishana mawazo, kupata  mahusiano mapya na kujenga mikakati,” alisema Bahati Muriga.

Nae aliyekuwa Mshiriki wa Shindano lala Mama Shujaa wa Chakula msimu wa nne Eva Mogeni akizungumzia Juu ya Safari hiyo alisema hii ni Fursa kwa wakulima wadogo wadogo kupaza sauti zao kuhusiana na kilimo, pia aliongeza Fursa hii aliyoipata kutoka Oxfam itakuwa ni Chachu kwake kujifunza mambo mapya na yenyekuleta maendeleo zaidi.

Edina Kiogwe ambaye alishiriki mashindano ya mwaka huu alisema anatarajia mafunzo atakayoyapata yatamjenga na kumwongezea ujuzi zaidi, lakini pia aliwahamasisha wakulima wanawake wadogowadogo kujituma na kujitoa katika mashindano mbalimbali ili kupaza sauti zao na kupata fursa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...