Sunday, May 29, 2011

Siku Deogratius Temba alipofunga ndoa na Sylvia Rwanyamva

MAI 21, 2011 itabaki kuwa kumbukumbu ya milele kwa mwanahabari Deogratius Temba mkewe Sylvia Rwanyamva baada ya kufunga pingu za maisha.
Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofayika katika Ukumbi wa King Palace Sinza Kamanyora.



Deogratius Temba akiwa na mkewe Sylvia katika pozi eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam mara baada ya kufunga ndoa Mai 21, 2011.




"Riambe, riamaye..." "Kunywa baba, kunywa mama..." Kwa mila za kichaga anakotoka bwana harusi ukikaribishwa nyumbani kiheshima lazima upewe pombe aina ya mbege unywe kidogo. Hapa maharusi wakinywa mbege baada ya kuingia ukumbini kukaribishwa uchagani.

Cheki pozi hili...duh, wanapendeza, Mungu aendelee kuwalinda mkae katika upendo milele. 
********
Bwana harusi ni Ofisa Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) huku mkewe ni mfanyakazi wa Benki ya Access Tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Blog ya Harusi na Matukio inawapongeza na kuwatakia maisha mema, marefu na yenye mafanikio.



No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...