Sunday, May 15, 2011

Harusi ya EDSON Ishengoma na JOVINA John

Edson Ishengoma (wapili kushoto) akiwa na mkewe Jovina John (wa pili kulia) pembeni mwao ni wasimamizi wao.


Edson na mkewe Jovina wakipiga picha ya ukumbusho na mama mzazi wa bwana harusi, Geraldina Ishengoma (wa kwanza kulia) muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa Katoliki Tegeta jijini Dar es Salaam. Waliosimama mbele ni wapambe wa harusi hiyo. 


Katika harusi nyingi ni mara chache hii kutokea, Pichani Bwana harusi Edson akimuendesha mkewe, wakiwasili katika Ukumbi wa Camp David Tegeta jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo hafla hiyo kabambe ilipofanyika Mei 14.

Dani ya Ukumbi wa Camp David; hapa ndio mahali maalumu ambapo maharusi waliketi.

Wapambe wa maharusi wakisafisha njia kuingia ukumbini kabla ya kuingia maharusi, Edson na Jovina.

Edson na mkewe Jovina wakiingia ndani ya Ukumbi wa Camp David kwa staili ya aina yake.


Mwanamama maalumu aliyeandaliwa akishusha baraka (sala) ndani ya ukumbi kabla ya shughuli za hafla hiyo kuendelea.


Mratibu wa hafla hiyo (floor manager), Bw. Samuel akiwakaribisha rasmi wageni waalikwa kwenye hafla hiyo, pembeni yake ni msema chochote maharufu, DC Kashasha (MC) ambaye ndiye alieongoza shughuli nzima ukumbini. 



Mama Geraldina Ishengoma akishauriana jambo na shangazi yake na Edson, Mrs Ewald Mushi. 


Picha ya kushoto ni dada wa bwana harusi, Janeth Ishengoma (wa kwanza kulia) akiingia ukumbini. Picha ya kulia Janeth akimpongeza mama yake, Geraldina Ishengoma baada ya kutoa nasaha kwa maharusi.



Wasimamizi wa harusi ya Edson na Jovina wakiwa katika pozi ukumbini.


Meza ya wazazi wa bwana harusi, Edson


Baadhi ya wageni waalikwa wakifurahia moja ya matukio katika hafla hiyo


Baadhi ya ndugu wa bwana harusi, Edson wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla hiyo




Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea na utaratibu wa 'kata mti panda'. Juu yao ni moja ya screen kubwa ambazo zilikuwa pande mbalimbali za ukumbi huo zikionesha matukio yote 'live' wakati hafla ikiendelea.
Picha zaidi za harusi hii tembelea gazeti la mtandao:- http://thehabari.com/ mtandao mshirika wa Harusi na Matukio. Lakini kama una picha za harusi tutumie matukio@thehabari.com


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...