Wawezeshaji wa kisheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuzungumza na wafanyabishara wa Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam, kuhusu masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji Sheria, Tamasha Amri kutoka Soko la Temeke akielezea masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji Hadija Mohamed akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria, Joanitha Katunzi kutoka Soko la Temeke akielezea ukatili wa kijinsia unaopingwa.
Mwezeshaji Sheria, Zainabu Namajojo, akizungumza na wanafanyabiashara.
Wafanyabiashara wakipata mafunzo.
Ofisa Usalama wa Soko hilo, Nurdin Hassan akizungumza na wafanyabiashara.
Mwezeshaji Sheria, Mariam Rashid akichangia jambo.
Bibi Fatma Mohamed akiuliza swali.
Mwezeshaji Sheria, Joanitha Katunzi kutoka Soko la Temeke, akimuelekeza jambo Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Susan Sitta.
Mafunzo yakiendelea.
Mfanyabiashara Boaz Iddi akiuliza swali.
Bi.Hidaya Iddi akiuliza swali.
Maswali yakiulizwa.
Mwonekano wa Soko la Feri.
Mwezeshaji wa Kisheria katika Soko la Tabata Muslimu, akizungumza na wafanyabiashara.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHARA wa Soko la Kimataifa la Samaki la Feri wametakiwa kuacha kufanya ukatili wa kijinsia wa kiuchumi ili kila mmoja wao apate fursa ya kufanyabiashara katika mazingira bora.
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mwezeshaji wa Kisheria kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Mariam Rashid kutoka Soko la Kigogo Sambusa wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni akiwa ameambatana na wawezeshaji sheria wenzake na viongozi kadhaa wa shirika hilo.
"Nawaombeni wanaume na wanawake acheni vitendo vya ukatili wa kijinsia wa uchumi kwani unarudisha nyuma maendeleo yenu na kuyafanya mazingira yenu ya kufanyia
biashara kuwa si rafiki" alisema Rashid.
Alitaja ukatili wa kiuchumi ni mtu kwenda kuchukua bidhaa ya mwenzake na kuondoka nayo kinguvu bila ya kulipia au mtu kula chakula cha mama lishe na kukataa kumlipa fedha yake.
Rashid alitaja aina za ukatili wa kijinsia kuwa ni ukati wa kingono,kiuchumi, lugha chafu pamoja na kisaikolojia.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma alisema vitendo vya kujambisha,dunga dunga, kuvuta sigara kwenye kadamnasi na kumshika mtu kwenye
maungo yake bila ridhaa yake ni ukatili wa kijinsia ambao unapigwa vita katika kampeni inayoendeshwa na EfG.
Alisema suala la wanawake kuvaa nguo fupi na wao kuanza kuwazomea na kuwashika maungoni ni kosa kisheria kwani hapa nchini hakuna sheria iliyoelekeza nguo ya kuvaa kutokana na soko hilo kuingia wageni mbalimbali kutoka mataifa mengine kama Bara la Ulaya na Afrika ambao wengine hawana mipaka ya kuvaa nguo zao.
Aliongeza kuwa jambo la kushangaza wanaofanyiwa vitendo hivyo ni wanawake wa hapa nyumbani lakini wageni hata wakiwa wamevaa nguo hizo fupi hawafanyiwi vitendo
hivyo.
Mfanyabiashara katika soko hilo Boaz Iddi alisema uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake wanaokwenda kupata mahitaji katika soko hilo unachangia vijana kuingiwa na tamaa
na kujikuta wakiwashika sehemu za mwili wao.
"Hawa dada zetu ndio wanaotuingiza katika matamanio kutokana na mavazi yao mafupi wanayoyavaa wakija katika soko hili" alisema Iddi.
Katika hatua nyingine wafanyabiashara wa soko hilo wamewalalamikia Askari wa Suma JKT wanaoangalia usalama katika soko hilo kuwa wamekuwa wakiwafanyia ukatili wa
kijinsia kwa kuwapiga baadhi yao wanapokuwa wamefanya makosa mbalimbali katika soko hilo.
Wafanyabiashara hao walidai kuwa hivi sasa katika soko hilo hali sio shwari kutokana na askari hao ambao wamekuwa wakitoa vipigo na adhabu za kijeshi kwa raia lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao ambapo wamefikia hatua ya kutoza ushuru mtu anapoingia na baiskeli na wale wanaobainika wakiuza maji na mifuko ndani ya soko hilo.
"Tunashindwa kuelewa hii hali ya hawa askari itakwisha lini hatuna raha kabisa katika soko hili tangu waanzekazi askari hawa Rais John Magufuli alisema wafanyabiashara tusibughuziwe lakini hali imekuwa ni kinyume katika soko hili huu ni ukatili wa kijinsia tunaofanyiwa na askari hawa" alisema mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.
Mmoja wa maofisa usalama wa soko hilo Nuordin Hassan akizungumzia suala hilo alisema kuna umuhimu wa kuwepo kwa mazingira rafiki kati ya askari hao na wafanyabiashara ili kazi ziendelee kufanyika bila ya kuwepo kwa changamoto zozote.
"Awali hali hii haikuwepo kwa sababu waliokuwa wakisimamia usalama katika soko ni walinzi shirikishi lakini hawa wakimkamata mtu ni kumpa adhabu kali mtuhumiwa jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa karibu" alisema Hassan.
Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Susan Sitta alisema lengo la kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu kupinga vitendo hivyo ni kuwaongezea uelewa ili waweze kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko na kutoa fursa kwao kufanya biashara zao kwenye mazingira rafiki.
Sitta alisema mradi unaoendesha kampeni hiyo ya Mpe Riziki si Matusi umefadhiliwa na Shirika la United Nations Trust Fund na kuwa unafanyika katika masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Temeke.
No comments:
Post a Comment