Monday, October 2, 2017

Benki ya NMB yazindua wiki ya huduma kwa wateja, yaahidi kuboresha huduma

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akizindua Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kuliruhusu gari la huduma kwa wateja kuzunguka kutoa huduma maeneo mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akiwatunuku baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo vyeti vya utendaji kazi bora katika kuwahudumia wateja wao mbalimbali.

  BENKI ya NMB Tanzania imezindua wiki ya huduma kwa wateja ambapo imeahidi kuboresha zaidi huduma kwa wateja wake wa sasa na kuwafikia wananchi ambao bado hawajapata huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja na kusema kila mwaka wamekuwa wakiboresha huduma mbalimbali ambazo zinatolewa sasa na kuanzisha zingine mpya na wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuboresha huduma hizo. “Kila mwaka ni mzuri sababu kunakuwa na jambo tofauti pamoja na hilo pia tupo katika nafasi nzuri kama benki namba moja Tanzania, ni jambo la kujipongeza sababu tulipo sasa sio sawa na miaka 12 iliyopita, “Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha huduma zetu na zaidi kidigitali ili kuahisha huduma za kifedha kuwepo karibu zaidi na wateja wetu, huduma ya kidigitali inahitaji huduma ya intrnet ambayo kwa sasa nchini ipo vizuri na simu ya kisasa (smartphone) ambazo hata gharama zake kwa sasa zipo chini," amesema Ineke na kuongeza. “Tumekuwa tukitoa huduma boa lakini pamoja na hilo hatuwezi kuwafikia wateja wote ndiyo maana tumekuwa na mawakala zaidi ya 3,500 nchi nzima ambao wamekuwa wakitoa huduma kwa wateja wetu." Aidha Ineke amesema moja ya changamoto ambayo benki imekuwa ikikutana nayo kwasasa ni huduma za kifedha kupatikana kupitia mitandao hivyo wateja wengine kutumia mitandao yao kuhifadg=hi pesa lakini wamejipanga kuja na njia mbadala ikiwa na huduma bora zaidi ambazo zitawashawishi wananchi kutumia benki kutuma fedha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akiwatunuku baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo vyeti vya utendaji kazi bora katika kuwahudumia wateja wao mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akiwatunuku baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo vyeti vya utendaji kazi bora katika kuwahudumia wateja wao mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker akiwatunuku baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo vyeti vya utendaji kazi bora katika kuwahudumia wateja wao mbalimbali.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania, Ineke Bussemaker (hayupo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...