Mwalimu wa shule ya Msingi
Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza
zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku
hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la
Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa
wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali.
Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima
macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali
Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku
hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la
Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa
wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali.
Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics
inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima.
Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics
inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima.
Zoezi la Uandikishaji wa majina wanafunzi wa shule ya Msingi Nguvumali kwa ajili ya upimaji wa macho likiendelea.
Zoezi la kuwapima wanafunzi likiendelea |
SABABU
kubwa za wanafunzi wa shule za msingi kutokufanya vizuri darasani
imeelezwa inatokana na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana
akili .
Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15
wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na
kushindwa kufikia malengo yao.
Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani
Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda
sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics
inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.
Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi
kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za
utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.
“Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa
wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na
hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika
kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.
Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa
asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na
virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.
Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita
limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni
na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia
matitabu zaidi na kampuni hiyo.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Noor Optics,
Raouf Nasser alisema lengo kubwa ni kutoa huduma hiyo katika shule zote za
msingi ili kusaidia kubaini changamoto za macho zinazowakabili na namna ya
kupatiwa ufumbuzi.
Alisema alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na
halmashauri ya Jiji la Tanga wameamua kuendesha zoezi hilo kila mwaka ili
kuweza kuwasaidia watoto ambao watabainika wanakabiliwa na matatizo hayo ili
waweze kufikishwa kwa wataalamu kwa matibabu zaidi.
“Asilimia kubwa ya wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka
watoto wao katika hospitali kufanyiwa vipimo vya matatizo hayo hivyo sisi
tumeamua kwa nia moja kusaidia jamii ikiwa ni kurudisha faida kwao kutokana na
huduma tunazotoa “Alisema.
Aidha alisema msingi mzuri wa kuyatunza macho ni lazima
kuwepo utaratibu wa kuyafanyia vipimo mara kwa mara hasa wanapokuwa kwenye
hatua ya ukuaji kabla ya kufikia umri mkubwa ambapo tatizo hilo linaweza kuwa
kubwa zaidi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment