Monday, October 30, 2017

Mchekeshaji maarufu Joti atia fora 'miuno' siku ya harusi yake

Mchekeshaji maarufu wa Kundi la Orijino Komedi nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti akiwa na mkewe Bi. Tumaini Salehe mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Joti na mkewe akiwa na wapambe wake.

  MCHEKESHAJI maarufu nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti huenda akaingia katika kumbukumbu ya mwaka 2017 kuwa bwana harusi aliyecheza muziki akikata viuno kuliko maharusi wowote. Joti ambaye ni mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi, alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Bi. Tumaini Salehe katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

 Mchekeshaji huyo akiwa katika sherehe ya ndoa yake iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, aliongoza kwa kusakata rumba mwanzo mwisho jambo ambalo lilikuwa burudani tosha katika hafla hiyo.

"..Yaani jamani harusi ya leo ni kama show ya Joti...mwanzo mwisho ni kucheza," alisema mwanadada mmoja aliyeshiriki katika harusi hiyo. Katika harusi hiyo, Joti ambaye alikuwa katika muonekano wa mnyoo wa kiduku aliwavunja mbavu waalikwa kutokana na kucheza kwa vituko huku akimwaga miuno, tena mbele ya wakwe zake jambo lilioufanya mkumbi kufurahia kitendo hicho mara zote.

 Joti alimwaga miuno hadi kuona koti la suti yake linamzuia mara kadhaa hivyo kulivua na kuliweka pembeni ili amwage mauno sawasawa. Kundi la wana Orijino Komedi ambao nao walimuunga mkono mwenzao walitoa 'show' kali ya kumwaga miuno kwa zamu ambapo walimuinua tena Joti alipoketi na mkewe na kuendelea kumwaga miuno, kabla ya kuingia tena mwimbaji maarufu wa muziki wa dansi, Christian Bella ambaye pia alimchezesha Joti kana kwamba waliandaa show ya kuwaburudisha waalikwa wake.

 "..Yaani leo bwana harusi huyu atalala hoi...si kwa miuno hii," alisema dada mmoja akiwa anachukua video kwa kutumia simu yake. Kwa historia hiyo huwenda Joti akawa bwana harusi pekee aliyecheza kwa muda mrefu tangu kuanza kwa sherehe yake hadi mwisho.

Bi. Tumaini Salehe siku ya send off akiwa na mumewe mtarajiwa.

Mchekeshaji maarufu wa Kundi la Orijino Komedi nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti akiwa na mkewe Bi. Tumaini Salehe mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...