Tuesday, May 10, 2016

Tozo Daraja la Nyerere Kuanza Rasmi Jumamosi

Daraja Kigamboni Daraja Kigamboni[/caption] Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza rasmi tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyererejijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, amesema kuwa tozo hizo zitaanza kutumika rasmi Jumamosi wiki hii na zitahusisha vyombo vyote vya usafiri. “Hakikisheni mnazifahamu tozo zote zitazotumika katika daraja hili kwa magari ya aina zote ili kuondoa usumbufu wakati wa utekelezaji wa zoezi la malipo”, Amesema Eng. Nyamhanga.

 [caption id="attachment_71549" align="alignnone" width="640"]KatibuMkuuwaWizarayaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), akitangazarasmitozozitakazotumikakwamagariyatakayovukadaraja la NyererekuanziaJumamosi wiki hii. KuliakwakeniMkurugenziMkuuwaUwekezajikutokaMfukowaHifadhiyaJamii(N.S.S.F), YacoubKidula. KatibuMkuuwaWizarayaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), akitangazarasmitozozitakazotumikakwamagariyatakayovukadaraja la NyererekuanziaJumamosi wiki hii. KuliakwakeniMkurugenziMkuuwaUwekezajikutokaMfukowaHifadhiyaJamii(N.S.S.F), YacoubKidula.[/caption] Katibu Mkuu huyo amezitaja tozo hizo kuwa ni pikipiki zitatozwa shilingi 600, mikoteteni, Guta, Bajaji, na magari madogo yatatozwa shilingi 1500, wakati magari aina ya ‘pick up’ yatakayozidi tani mbili na mashangingi yatatozwa shilingi 2000. Amefafanua kuwa mabasi yanayo beba abiria wasiozidi 15 (mini bus) yatatozwa shilingi 3000, mabasi yanayobeba abiria kuanzia 15 hadi 29 yatatozwa shilingi 5000. Mabasi yanayobeba abiria zaidi ya 29, Trekta na magari makubwa yenye uzito wa tani 2-7 yatatozwa shilingi 7000. Ameongeza kuwa matrekta yenye matrela, magari makubwa yenye uzito wa tani saba hadi 15 yatatozwa shilingi 10,000 wakati magari yenye uzito wa tani 15 hadi 20 yatatozwa shilingi 15,000. Katibu Mkuu Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye uzito usio wa kawaida (abnormal load) yatapita kwa vibali maalum vinavyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na kusisitiza kuwa tozo zote zimezingatia maoni ya wadau na hali ya uchumi wa wananchi ili kumudu gharama za matumizi ya daraja hilo. [caption id="attachment_71550" align="alignnone" width="640"]RaismstaafuwaawamuyaNne JakayaMrishoKikwete,akifafanuajambokwaKatibuMkuuwaWizarayaUjenzi, UchukuzinaMawasiliano (Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia),wakatiakiendeleanaukaguzikatikadaraja la Nyerere.KushotoniMkuuwaMkoawa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda. RaismstaafuwaawamuyaNne Jakaya Mrisho Kikwete, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara  ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), wakati akiendelea na ukaguzi katikadaraja la Nyerere.KushotoniMkuuwaMkoawa Dar es salaam Paul Makonda.[/caption] “Magari yote ya Serikali na taasisi za umma yatatakiwa kulipa tozo kama ilivyo bainishwa isipokuwa yale yenye namba za jeshi (Magereza, Polisi, JWTZ, Zimamoto) na magari ya wagonjwa”, amesisitiza Eng. Nyamhanga. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Uwekezaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (N.S.S.F), Yacoub Kidula, amewataka wananchi kuchangia gharama za uendeshaji wa daraja hilo ili kuongeza mapato ya Serikali. Takribani wiki tatu magari yamekuwa yakivuka katika Daraja la Nyerere bila tozo ambalo lilifunguliwa katikati ya mwezi Aprili mwaka huu na Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...