Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara
ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim
Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya
siku ya madansa duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisa Mwandamizi Masoko
na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto) akimkabidhi fulana, Jumanne Mnola alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa
duniani iliyofanyika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto), akimkabidhi fulana mmoja wa wateja wao, Said Ally, alipotembelea
banda lao wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika kwenye
viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko
na Uhusiano (Nssf), Amina Mbaga akigawa vipeperushi kwa baadhi ya
wananchi waliotembelea banda lao.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Faides Mdee, akigawa vipeperushi
kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika uzinduzi wa siku ya
madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dares Salaam, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na NSSF.
Wafanyakazi wa NSSF
wakimkabidhi fulana mteja wao, Antela Salumu (katikati).
Ofisa wa
NSSF, Innocent Shao, (kulia) akiwaandikisha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF walipotembelea banda la NSSF katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyoadhimishwa kwenye
viwanja vya TCC Club Chang’ombe na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa
uandikishaji NSSF, Amina Kisawaga (kulia) akitoa maelezo kwa mteja alietembelea
banda lao Fumbwe Juma, katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment