Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika wilayani Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa (nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.
Na Dixon Busagaga
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko
wilayani Kahama umetiliana saini hatii ya makubaliano ya Dola 200,000 sawa na shilingi
Milioni 440 za Tanzania na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) kwa ajili ya
mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto katika wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga
Mgodi
Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia na Taasisi ya Benjamin
W. Mkapa (BMF) wamesaini hati ya makubaliano ili kushirikiana katika kutekeleza
mradi wa miaka miwili unaolenga kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto
katika jamii .
Mgodi wa Bulyanhulu kupitia Mfuko wa
Maendeleo wa Acacia utatoa kiasi cha dola za Kimarekani 200,000 kusaidia awamu
ya pili ya mradi wa BMF utakaosaidia kuboresha huduma ya vituo viwili vya afya
wilayani humo, Kituo cha Afya cha Bugarama na Zahanati ya Kakola kupitia mradi
huo.
Mradi huo katika vituo tajwa
unatarajiwa kunufaisha wananchi 321,852 katika Halmashauri ya Msalala ambapo makubaliano
hayo ya miaka miwili yanaanzia, 01 April 2016 hadi 30 Machi 2018.
“Mgodi wetu unaendesha shughuli zake
katika halmashauri ya Msalala hapa mkoani Shinyanga na sehemu ya uwajibikaji
wetu kwenye jamii, kupitia mkakati wa mipango endelevu kwenye jamii na kusaidia
mikakati ya uboreshaji wa sekta ya afya kwa ajili ya jamii inayozunguka mgodi.”alisema
Graham Crew.
“Ushirikiano huu na Taasisi ya BMF
umekuja wakati muafaka ambapo BGML imewekeza katika miundombinu ya kuipandisha
hadhi zahanati ya Bugarama kuwa kituo cha afya na pia kumalizia ujenzi wa
Zahanati ya Kakola.” Aliongeza meneja huyo mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew.
Awamu ya pili ya Mradi wa BMF
inalenga kutekeleza mradi utakaoboresha huduma za HIV/AIDS, huduma za mama na
mtoto kwa kuongeza upatikanaji wa wataalamu wa afya na kuboresha miundombinu ya
kutolea huduma za afya.
Afisa Mtendaji Mkuu wa BMF Dk Ellen
Mkondya Senkoro amesema; “Takwimu zinaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga una
maambukizi kwa asilimia 7.4% ambapo kiwango kikubwa kipo katika halmashauri ya
Msalala kutokana na shughuli za uchimbaji madini hasa uchimbaji mdogo mdogo.”
“Kiwango hiki kimeendelea kuwa hivyo
tangu mwaka 2007/2008 hadi 2011/2012 ingawa kiwango cha maambukizi nchini
kimepungua kutoka asilimia 5.7% hadi 5.1% hivyo sehemu hii inahitaji hatua
maalumu. “alisema Dkt Mkondya.
Alishukuru Kampuni ya ACACIA kwa msaada huo na kwamba utasaidia kwenye
utekelezaji wa uboreshaji wa mifumo ya kukabiliana na tatizo la Virusi vya
Ukimwi, huduma za uzazi na watoto kwa kuongeza rasilimali watu ya watalaamu wa
afya, uendelezaji wa miundombinu na kujengea uwezo maeneo yanayohitaji ufanisi
zaidi.
Tangu mwaka 2013 Taasisi ya
Benjamin William Mkapa (BMF) imekuwa ikishirikiana na Acacia kupitia Mfuko wake
wa Acacia Maendeleo Fund katika kutekeleza sehemu ya miradi ya awamu ya pili ya
mfuko wa taasisi ya BMF katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na Halmashauri
iliyokuwa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa Acacia:
Mfuko wa Maendeleo wa Acacia maarufu
kama Acacia Maendeleo Fund ulianzishwa mwaka 2011 kama sehemu ya dhamira katika
kuboresha maendeleo endelevu katika jamii kwenye maeneo tunayofanya kazi. Hadi
sasa tumefanikiwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 35.0 katika miradi 150
kwenye maeneo mbalimbali.
Misaada kutoka kwenye mfuko huu hutoa
kipaumbele kwa vitega uchumi vinavyosaidia maendeleo ya jamii, ujengaji wa
uwezo, sekta ya afya, elimu, maji, mazingira katika maeneo tunakoendesha
shughuli zetu.
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ilianzishwa April 2006
na Rais Mtaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin W.
Mkapa, taasisi hii isiyo ya kiserikali ina dhamira ya kuboresha afya na hali za
watanzania hasa katika maeneo yaliyoko vijijini kwa kutekeleza miradi yenye
kutoa matokeo.
No comments:
Post a Comment