Sunday, May 29, 2016

Wabunge Wapimwa Afya Zao Mjini Dodoma...!

 Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA) katika Zahanati ya Bunge, Dodoma.

 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma.

 Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Sokombi akipimwa afaya na Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Asha Shao. Katikati ni muuguzi mwingine Christina Chamwela.

 Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Dodoma akimpima kimo Mbunge


 Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu akipimwa mapigo ya moyo.


 Mbunge Kanyasu akipimwa kimo

 Mbunge wa Jimbo la Nachingwe, Hassan Masala akipimwa kimo

 Mbunge wa Jimbo la Makambaku, Deo Sanga akipimwa afya

Baadhi ya wabunge wakipata ushauri nasaha

Harusi ya Bw. Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel Dar es Salaam



Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam leo May 28, 2016. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog -(Kajunason Studio).

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam. Pembeni ni wasimamizi wao.

Waumini waliohudhuria.

Mchungaji wa Kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam akifungisha ndoa ya Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel.

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakila kiapo.

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakila kiapo.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitoa sadaka.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini katika cheti kama shaidi wa ndoa hiyo mara baada ya Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel kufunga ndoa.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akiwapongeza maharusi.

Mchungaji wa kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam akiweka saidi katika cheti.
Maharusi wakipongezana kwa kupeana cheti.

Maharusi wakitoka kanisani.

Picha ya pamoja.

Pongezi.

Salamu za hapa na pale.

Wazazi wakiwapongeza watoto wao.

Uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016...!


 Masoud Kipanya, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus na mtangazaji wa kipindi hicho akizungumza  wakati wa hafla ya ufunguzi i liyofanyika jana usiku  katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU


 Masoud Kipanya, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus na mtangazaji wa kipindi hicho akifurahi jambo na washiriki wa vipindi vvilivyopita vya Maisha plus  wakati wa hafla ya ufunguzii liyofanyika katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU

                         Wasanii Vitali Maembe na Jhikoman wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

Mwanahabari na bloger John Bukuku akihojiwa na mtangazaji wa Azam Tv Benerick ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa maisha plus.

Waanzilishi wa kipindi cha Maisha plus Kaka Bonda na David Sevuri wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa kipindi cha maisha plus mapema jana usiku katika viwanja vya studio za  Azam Tv

Mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa vipindi vya maisha plus akihojiwa na mtangazaji wa Azam wakati wa ufunguzi wa msimu mpya wa Maisha plus East Afrika 2016 yenye kauli mbiu ya #HAPA KAZI TU

Mkurugenzi wa Azam Media  Tido Mhando (Kushoto) akiwa na Masoud Kipanya akiongea na wageni waaalikwa waliohudhuriia  uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016 ambaye itaoneshwa katika chaneli ya Azam TWo kuanzia jumapili hii saa tatu usiku .

Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakishuhudia ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa Maisha plus East Afrika 2016 yenye kauli mbiu ya #HAPA KAZI TU

Wawakilishi kutoka bodi ya filamu Tanzania wakifuatilia kwa makini  uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016 uliofanyika jana katika viwanja vya studio za Azam Tv 

 Aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Maisha Plus Abdul akizungumza katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika jana katika uzinduzi wa maisha plus wakifuatilia kwa makini 


Friday, May 20, 2016

Tigo Yazindua Huduma ya Tigo Games

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa  huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games jijini Dar Es Salaam jana.Tigo Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni  michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenye simu za Smartphone au Tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakua App ya Tigo Games.


Wasanii wakiigiza kama Mazombie katika kunogesha uzinduzi wa TIGO GAMES


Wasanii wakicheza mpira katika uzinduziwa tigo games mapema jana katika ukumbi wa High Spirit Jijini Dar es salaam


Wadau mbalimbaliwakipata taswira mbele ya gari katika RED carpert 




Wasanii wakiwa katika pozi na mfano wa Risasi katika uzinduzi wa TIGO GAMES 


Wadau wakifurahi jambo katika uzinduzi huo


Mtangazaji wa Choice Fm na Mchekeshaji Idris Sultan akiwa live jukwaani kusherehesha uzinduzi wa Tigo Games mapema jana katika ukumbi wa High spirit Jijini Dar es Salaam


Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akifurahi jambo na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) wakati wa uzinduzi 




Wasanii wakitumbuiza nyimbo za michael Jackson



Mfanyakazi wa Huawei akielekeza jinsi ya kucheza Games hizo mbalimbali zinazopatikana katika Tigo Games 


Baadhi ya wadau wakipata maelekezo jinsi ya kuingia katika mashindano ya kucheza Games na mshindi kujishindia Zawadi


Waandishi wa habari wakishindana kucheza Games katika uzinduzi wa Tigo Games jana usiku 


Msanii wa kizazi kipya Benpol akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa clouds tv Perfect baada ya uzinduzi wa tigo games


Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Tigo Games mapema jana usiku




Wadau wakipata picha katika sanamu za michezo ya Tigo Games 


Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Tigo Games 
 Kampuni ya simu inayoendesha maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, leo imetangaza uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games. Tigo Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni  michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenyeSmartphone au tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakuaApp ya Tigo Games. Kwa wateja wenye simu za kawaida zilizo na intaneti watapata huduma hii katika tovuti ya Tigo Games.
 Michezo zaidi ya 800 inapatikana kupitia huduma hii ikiwemo michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe, Zombie Run na Tokyo Drift.
 Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya  michezo  inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katikamitandao ya simu Tanzania  kutoa jukwaa la michezo linaloweza kutumiwa  na watu wengi ambapo wateja wa Tigo  wanaweza kucheza michezo mbalimbali  kulingana na chaguo lao kwa gharama wanayoimudu. Tigo imejikita kuendelea kusimamia maslahi ya wateja wake kwa kutoa  bidhaa nyingine nyingi  kwa ajili ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.”
 “Tigo sasa ndio inaongoza katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE nchini, na kwa sasa huduma hii inapatikana katika miji mikubwa 12. Tunaamini kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi zaidi itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akichajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezoaipendayo na kuicheza atakavyo wakati wowote.  Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi cha siku, wiki na hata mwezi; pia kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa mda wowote autakao bila makato yeyote. Malipo ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo hitajika. Uzinduzi wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo wateja wataweza kufurahia huduma bure 

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...