Saturday, September 22, 2012

Send Off ya Bi. Veronica Stima iliyofanyika Tabora

Send Off ya: Veronica Stima Ilifanyika: Ukumbi wa Student Centre,Tabora Rangi ya Send Off: Paple na Gold Tarehe: Septemba, 2012
Bibi Harusi mratajiwa Veronica Stima akisindikizwa na kaka yake, John Stima kuingia ukumbi kwa ajili ya sherehe ya kumuaga (Send Off) iliyofanyika Ukumbi wa Student Centre, Tabora.
 Baba na mama wa Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza nyimbo ya kabila lao (Kifipa).
 Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini.
 Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake aliomsindikiza katika sherehe ya Send Off Ukumbi wa Student Centre, Tabora.
 Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene kwa ishara ya upendo
Wachanga nao hawakuwa nyuma kuonesha umoja wao na ule wimbo wao wa kushikana mikono ('Iringi').
 Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica wakienda mbele ya wageni waalikwa kwa ajili ya utambulisho.
 ...Hapa akilishwa keki na mtarajiwa wake
 Bibi harusi mtarajiwa akiwaaga wazazi wake
 ...Bibi harusi mtarajiwa akitoa zawadi ya keki kwa mama mkwe mtarajiwa huku akisindikizwa na kaka yake.
 
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba wa bibi harusi mtarajiwa akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa.
Mama Catherine Stima ambaye ni mama mzazi wa bibi harusi naye alipata fursa ya kumuasa mwanaye.
 Kaka mkubwa John Stima akizungumza kabla ya zoezi la kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Wajua alisema nini...! sikiliza "Chonde chonde, nawakabidhi dada yangu mpendwa akiwa hana hata doa moja... nawaombeni msije mkanyanyasa huko kwenu...".
 
...mara baada ya maneno machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi.
 Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyo takikana.
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake.
 Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyoona hapa.
Na hii ni picha ya kumbukumbu kwa wake na watoto wao. Nguzo zote za shughuli hiyo zimedizainiwa na kushonwa na mwanamitindo Manju Msita

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...