Sunday, September 23, 2012

Maonesho ya Usiku wa Mitindo (Mitindo Night)

 Maonesho ya Usiku wa Mitindo (Mitindo Night) Mbalamwezi Beach.
Wabunifu wa mavazi katika usiku wa mitindo uliofanyika Mbalamwezi beach walikuwa ni Diana Magese, Mitindonite iliwakilishwa na Ally, Amin, Wancy na Matrida, Bambo collection, Renee, Cocoriko, William Johnson, Veronica Ruhenzi-VS collection, Dorcas, Subira, Salim Ally, na Wavisa Collection.


                        




Ma modo Mbalimbali wakipita katika Jukwaa



  MC katika maonyesho hayo  Ireene Tilya , akiwa anaendelea na kazi





Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa kwaribu maonesho hayo

Saturday, September 22, 2012

Send Off ya Bi. Veronica Stima iliyofanyika Tabora

Send Off ya: Veronica Stima Ilifanyika: Ukumbi wa Student Centre,Tabora Rangi ya Send Off: Paple na Gold Tarehe: Septemba, 2012
Bibi Harusi mratajiwa Veronica Stima akisindikizwa na kaka yake, John Stima kuingia ukumbi kwa ajili ya sherehe ya kumuaga (Send Off) iliyofanyika Ukumbi wa Student Centre, Tabora.
 Baba na mama wa Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza nyimbo ya kabila lao (Kifipa).
 Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini.
 Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake aliomsindikiza katika sherehe ya Send Off Ukumbi wa Student Centre, Tabora.
 Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene kwa ishara ya upendo
Wachanga nao hawakuwa nyuma kuonesha umoja wao na ule wimbo wao wa kushikana mikono ('Iringi').
 Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica wakienda mbele ya wageni waalikwa kwa ajili ya utambulisho.
 ...Hapa akilishwa keki na mtarajiwa wake
 Bibi harusi mtarajiwa akiwaaga wazazi wake
 ...Bibi harusi mtarajiwa akitoa zawadi ya keki kwa mama mkwe mtarajiwa huku akisindikizwa na kaka yake.
 
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba wa bibi harusi mtarajiwa akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa.
Mama Catherine Stima ambaye ni mama mzazi wa bibi harusi naye alipata fursa ya kumuasa mwanaye.
 Kaka mkubwa John Stima akizungumza kabla ya zoezi la kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Wajua alisema nini...! sikiliza "Chonde chonde, nawakabidhi dada yangu mpendwa akiwa hana hata doa moja... nawaombeni msije mkanyanyasa huko kwenu...".
 
...mara baada ya maneno machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi.
 Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyo takikana.
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake.
 Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyoona hapa.
Na hii ni picha ya kumbukumbu kwa wake na watoto wao. Nguzo zote za shughuli hiyo zimedizainiwa na kushonwa na mwanamitindo Manju Msita

Sunday, September 16, 2012

Harusi ya Mr Pascal na Florence Ernest

Harusi: Mr. Pascal na Florence
Kanisa: Moyo safi wa Bikira Maria Bagamoyo
Rangi: Orange na Chocolate
Sherehe: Ukumbi Kiramuu Mbezi Beach-Dar es Salaam
Tarehe: 14,September,2012.

Maharusi Bw. Pascal na Bi Florence wakiwasili ukumbini wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Moyo wa Bikira Maria, Bagamoyo mkoani Pwani na kufuatiwa na tafrija iliyofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.


 Maharusi Bw. Pascal na Bi Florence wakiwa pamoja na wasimamizi wao tayari kwa kupata mvinyo wa makaribisho.

 Bi harusi Florence akifurahia mvinyo ulioandaliwa kwa ajili yao katika ukumbi wa Kiramuu Septemba 14, 2012.

 Mtaarishaji maalumu wa ndafu akikatakata kwa ajili ya maharusi.

 Wazazi wa Bwana Harusi wakimlisha Bi. Harusi kipande cha ndafu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika familia yao.

 Mjomba wa Bw. Harusi, Lenny Kisarika (katikati) kulia ni mkewe na kushoto ni dada wa mjomba huyo.


Muandaaji Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio akisalimiana na mjomba wa Bw. Harusi, Mr. Kisarika na mkewe.


 Muandaaji Mkuu wa Blogu ya Harusi na Matukio akifurahia jambo na mjomba wa Bw. Harusi Mr. Kisarika na mkewe.

 Kaka wa Bi. Harusi (katikati) akiwa pamoja na familia yake na wanandugu wakipata kilaji.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwa makini!

 Muandaaji Mkuu wa Blogu ya Harusi na Matukio akifurahia jambo na Bi. Harusi Florence Ernest.

 Bi. Harusi akiselebuka pamoja na wageni waalikwa.


Wageni waalikwa wakeselebuka kwa mitindo mbalimbali ukumbini hapo.


Flowers wameremetile

Saturday, September 15, 2012

Harusi ya Mr Joachim Mushi na Hilder Mwaipopo

Ndoa kati ya :Mr Joachim Mushi na Hilder Mwaipopo
Ilifungwa  Kanisa : Kristu Mfalme Tabata
Rangi ya Harusi: Gold, Off white na Black
Ukumbi: King Palace Makuti hall Sinza
Tarehe: 25/08/2012.


 Kanisa la Kristu Mfalme Tabata ambalo ndilo maharusi hawa walifunga ndoa tarehe 25/08/2012 saa kumi alasili




Bwana harusi Bw. Joachim Mushi (Kulia) na Bi Hilder Kushoto wakiwa katika nadhili ya milele




 Pichani Maharusi wakivishana pete  ikiwa ni ishara ya uaminifu mpaka kifo kitakapo watenganisha.

 Maharusi Bw.Joachim Mushi na Bi. Hilder Mwaipopo wakiwa na nyuso za furaha na wakionesha shahada za ndoa







 Maharusi wakiwa katika Pose mbalimbali baada ya Kufunga ndoa katika kanisa la Kristu Mfalme Tabata Jijini Dar es salam



Maharusi wakiwa na wasimamizi wao  wa kwanza kulia ni Bw. Gide Magila na wa kwanza  kushoto ni Bi Adelgundis Magila.


 Maharusi wakiwa na nyuso za furaha wakiingia  ukumbini King Palace Makuti Hall Sinza


 Maharusi wakiwa na mvinyo na kushiriki na wageni waalikwa usiku wa tarehe 25/08/2012


 Maharusi wakifuatilia matukio katika hafla yakuwapngeza

 Flowers wakifurahia

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...