Wednesday, September 14, 2011

Harusi ya Ibra Kaude na mkewe Rahma Mohammed


"Mwenzagu Pokea pete hii iwe ishara ya upendo wangu kwako na uaminifu wangu kwao" Ndivyo inavyoonekana Rahma akisema wakati alipokuwa akimvisha pete ya ndoa mme wake, Ibra Kaude wakati wa Swala ya ndoa yao iliyofanyika Kigurunyembe mkoani Morogoro.


Ibra Kaude na mkewake Rahma Othumani Mohammed wakiingia ukumbini kwa madaha wakati  wakishiriki kwenye sherehe yao ya kuwapongeza iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, maharusi hao walifunga ndoa yao siku ya Septemba 9, 2011 katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe mkoani Morogoro.


Bwana Harusi Ibra Kaude na Rahma Othumani Mohammed, wakiwa katika pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao Septemba 9, 2011 mwaka huu katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-Hud uliopo Kigurunyembe mkoani Morogoro. Sherehe ya kuwapongeza ilifanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2011. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi  Vodacom Tanzania. (Picha zote na Mdau Albert Jackson)


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...