Tuesday, September 19, 2017

Utafiti matumizi bora na umiliki wa ardhi wafanyika Morogoro

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi (aliyesimama)akitoa maneno ya utangulizi kwa wadau wa Korido ya Mngeta na ukanda wa Magombela-Selous-Udzungwa wilayani Kilombero juu ya utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume hiyo wakishirikiana na Asasi ya kiraia ya African Wildlife Foundation uliolenga maeneo ya uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous, iliyofanyika Wilayani Kilombero.


Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife Foundation (AWF) ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous juu ya, utunzaji wa Mazingira na Bioanuai, Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.

 Wadau wakimsikiliza Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akiwasilisha utafiti huo.

 Bi. Jane Mkinga Afisa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania akichangia maswala juu ya maliasili.

 Diwani wa kata ya Mngeta Mh. Flora Kigawa akitaka kupata ufafanuzi  wa changamoto za kutatua migogoro kati ya vijiji na pia kutaka kufahamu idadi ya wanawake wangapi wanamiliki ardhi katika wilayani Kilombero.

 Diwani wa Kata ya Chita Mh. Chelele John akiuliza maswala mbalimbali yahusuyo Ardhi.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wadau kuhusu utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.

 Bw. Pastor Magingi Meneja wa Programu wa  asasi yakiraia ya African Wildlife Foundation akieleza namna walivyoshirikiana  NLUPC katika utafiti wa uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous.

 Muwezeshaji wa Mkutano huo Bw. Geofrey Siima akiendelea kutoa Muongozo wakati wa warsha hiyo.

 Afisa Miradi kutoka asasi ya Kiraia ya Solidardad Bi. Maria Sengelela akitoa maelezo ya namna wanavyoshirikiana na NLUPC katika swala zima la matumizi bora ya Ardhi.

Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Bi. Devotha Salukele akijibu Maswala mbali mbali yahusuyo sheria yaliyoulizwa na wananchi kuhusu Ardhi.

Afisa Ardhi Mteule kutoka Wilaya  Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akifafanua na  kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa mkutano huo.

 Afisa Mipango wa Wilaya ya Kilombero Bw. Ludwing Ngakoka akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mh. David Lugazio akitoa neno la Shukurani baada ya Mkutano huo kumalizika.


Wajumbe mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo
Picha ya pamoja 



KATIKA kuhakikisha kuwa kuna mipango na matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania, Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya African Wildlife Foundation (AWF) walifanya utafiti wa uhifadhi wa Mazingira, Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimila na Bioanuai katika korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous Wilayani Kilombero.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha utafiti huo kwa Madiwani, Watendaji Wilaya, Tarafa na Kata, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa Tume ilifanya utafiti katika ushoroba wa Mngeta pamoja na ukanda wa Udzungwa-Magombela-Selous lengo likiwa ni kuangalia mambo mbalimbali yanayohusu matumizi bora ya Ardhi, umiliki wa ardhi, uhifadhi ya mazingira na Bioanoai katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu alidokeza kuwa Wilaya ya Kilombero ni moja ya Wilaya tajiri katika nchi ya Tanzania ambayo ina ardhi yenye rotuba kubwa inayofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali pamoja na uoto wa aina mbalimbali “Kuna matumizi ya aina mbalimbali ya ardhi katika Wilaya hii, tuna wakulima, wawekezaji wakubwa katika kilimo, wawekezaji wakubwa katika misitu, hifadhi ya wanyama pori, kilomo cha kati na kilimo cha wakulima wadogo wadogo, wafugaji, wavuvi, wafanya biashara ambao kwa umoja wanatengeneza ubia mbalimbali katika matumizi ya Ardhi” alisema Dkt. Nindi.

Aliongeza kuwa lengo la utafiti huu ilikuwa kuangalia wadau mbalimbali katika utumiaji, upangaji na usimamizi wa ardhi wanatekelezaje, kuangalia changamoto za mipango ya matumizi ya Ardhi, umiliki wa ardhi,uhifadhi wa mazingira na Bioanoai.

“Tupo hapa kwa ajili ya kuwasilisha utafiti wetu kwamba namna gani mambo haya yanafanyika shughuli hizi za uhifadhi wa mazingira na Bioanoai, Shughuli za upangaji na matumizi ya Ardhi, umiliki wa Adhi pamoja na utekelezaji wake na usimamizi zinavyofanyika katika kanda hizi mbili” alisema Dkt. Nindi.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtaalamu wa mazingira kutoka Tume bwana Eugen Cyrilo, alibainisha changamoto kadhaa matumizi ya ardhi, umiliki pamoja na uhifadhi wa mazingira. “Changamoto kubwa iliyobainika katika utafiti huu, ni utekelezaji wa maipango ya matumizi ya ardhi. Vijiji vingi tulivyopitia vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi, ila kwa kuwa hakuna usimamizi wa mipango hiyo kwa ngazi ya vijiji, kunakuwa hakuna utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi waliojitengea” alieleza bwana Cyrilo.

Aidha, katika upande wa mazingira, ilibainika kuwa kumekuwa usimamizi usioridhisha hasa kwenye misitu na vyanzo vya maji kwa baadhi wanavijiji wenyewe au watu kutoka nje ya vijiji kuvamia na kuweka makazi kwenye misitu ikiwa pamoja na kukata miti bila utaratibu. “Kwenye baadhi ya maeneo, kumekuwa na uvamizi wa misitu ambapo hapo awali ilikuwa imetengwa kwa ajili ya uhifadhi, na sehemu zingine tulikuta wanavijiji wakifanya shughuli ambazo si rafiki kwa mazingira pembezoni mwa mito, hii ni tishio kubwa katika utunzaji wa mazingira” alisema bwana Cyrilo.

Akichangia katika matokeo ya utafiti huo, Meneja wa Programu kutoka AWF bwana Pastor Magingi aliwasihi uongozi wa Wilaya kuja na suluhisho la kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi ili kufanya kazi nguvu kubwa inayofanywa na na Tume, Wadau pamoja na Halmashauri yenyewe isipotee bure.

Hatua hii iliwapelekea Madiwani wa Kata zilizohusika kwenye utafiti huu kupendekeza kuwapo kwa mtaalamu wa Wilaya atakayehusika moja moja na kusimamia utekelezakji  wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya ili kutoa ripoti ya mara kwa mara juu ya usimamaizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ili kuwa endelevu na yenye manufaa kwa wananchi.

Utafiti huo ulihusisha Kata nne za ukanda wa Udzungwa-Magombera-Selous, ambazo ni Msolwa Stesheni, Mkula, Mang'ula B na Sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni, Mkula, Sonjo, Msufini,Katurukila, Kanyenja, Magombera na Sanje. Aidha katika korido ya Mngeta utafiti huo ulihusisha kata sita za Namawala, Igima, Mbingu, Mngeta, Chita na Mofu pamoja na Vijiji  vya Mofu, Ihenga, Kisegese, Vigaeni, Makutano, Igima, Mbingu, Njage, Mngeta, Mchombe na Lukolongo.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...