Mhudumu akiweka chupa ya Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza juzi. |
|
Muonekano wa Chupa |
Wagon waalikwa wakiwa wanafuatilia shughuli za uzinduzi |
Muda wa kuonja ladha ya Pilsner King mara baada ya uzinduzi mapema jana usiku katika Hotel |
Wagon waalikwa wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa pilsner king |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa katika picha ya pamoja na mwageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa pilsner king mapema jana usiku Jijini Mwanza. |
Mwanza, Septemba 20, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua bia mpya
inayojulikana kama Pilsner King ambayo ni mwendelezo wa bia ya Pilsner Lager iliyozoeleka
na ambayo ipo sokoni kwa kipindi kirefu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa bia hiyo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL
Cesear Mloka aliielezea bia hiyo mpya kama bia imara ambayo itakuwa kipenzi cha
wanaume jasiri na wanaojiamini.
Bia ya Pilsner
King ina kilevi cha asilimia 7.6%, na ndiyo bia imara kuliko zote
zinazozalishwa hapa nchini.
Mkurugenzi
huyo alifafanua kuwa, Pilsner King imetengenezwa na mzalishaji bia wa
Kitanzania kwa kanuni za kimataifa akitumia malighafi za hapa nchini zenye
ubora wa hali ya juu ambazo zimeipa bia hiyo ladha murua. “Hii ni kama zawadi
kwa wanaume wa kweli baada ya shughuli nyingi za mchana kutwa,” anasema Mloka
Kwa mujibu wa
mkurugenzi huyo, bia ya Pilsner imepata jina lake kutoka katika mji wa Pilsen
uliopo Jamuhuri ya Czech ambako bia hiyo ilitengenezwa kwa mara ya kwanza na
kuongeza kuwa, bia hiyo ya kipekee na yenye ladha ya aina yake itakuwa ni
chaguo sahihi kwa wateja wanaopenda kuwa ‘wanaume wa kweli’
“Ikiwa na kilevi cha asilimia 7.6% Alc,
Pilsner King, ambayo kauli mbiu yake ni ‘Kutana na Mfalme, kwa ajili ya Wanaume
Imara na Wenye Ujasiri’, imetengenezwa kwa kuzingatia kanuni halisi za
utengezaji wa bia ya kwanza ya Pilsner iliyotengenezwa huko Ulaya Mashariki,”
anaeleza Mloka
Uzinduzi huo
Ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, ambaye aliisifia kampuni
ya SBL kwa kuonyesha njia katika ubunifu wa vinywaji vyenye kileo hapa nchini.
Mongela pia
aliipongeza SBL kwa kufanya uwekezaji Mkoani Mwanza kupitia kiwanda chake cha
bia ambacho amesema kimekuwa kikichangia maendeleo ya kiuchuni ya mkoa huo.
“Napenda
kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa Mwanza kwa kampuni ya SBL. Uwekezaji wao hapa
Mwanza umesaidia upatikanaji wa ajira za
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja pamoja na fursa za kibiashara kwa
wakazi wa jiji hili,” alisema Mongela.
Pamoja na
kiwanda cha Mwanza, SBL ina viwanda vingine viwili vya bia, kimoja kipo jijijni
Dar es Salaam na kingine kipo Moshi mkoani Kilimanjaro. SBL inazalisha bia kama
vile Pilsner
Lager, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness Stout and bia inayobeba
bendera ya kampuni, Serengeti Premium ambayo imeshinda zaidi ya medali 10 za
kitaifa na Kimataifa.
No comments:
Post a Comment