Friday, September 29, 2017

Asasi za Kiraia Zanzibar zawafunda raia juu ya Utetezi na Ushawishi Sera

 Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuelekea katika vijiji viwili tofauti vya Msowelo na Matombo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.  


 Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao.

  Kundi lililokuwa likielekea Matombo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
 Wakiwasili Msowelo
Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar zimeendelea na mafunzo ya siku mbili kuhusu Utetezi na Ushawishi wa Sera mkoani Morogoro. Asasi mbalimbali kutoka Zanzibar na Pemba ziko katika ziara ya Mafunzo iliyoratibiwa na Foundation for Civil Society (FCS) chini ya mwamvuli wa Association of Non Governmental Organizations of Zanzibar (ANGOZA) inakutanisha wawakilishi Zaidi ya 40 kutoka Zanzibar ambao wamekuja kujifunza namna mashirika ya MVIWATA (Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal Center).
Katika siku ya pili washiriki hawa wamepata fursa ya kwenda uwandani ili kukutana na wanufaika wa kazi mbalimbali zinazofanywa na MVIWATA na MPLC. MVIWATA imewapeleka washiriki wilayani Kilosa katika kijiji cha Msowelo ambapo kijijini hapa kumekuwa na migogoro ya Wkulima na Wfugaji ambapo kijijini hapa MVIWATA imefanikiwa kutumia mtandao wake wa msingi kupaza sauti kwa serikali ili kutenga maeneo ya wakulima. Tayari wilayani hapa kuna mashamba 9, ambayo yamefutwa na yamekabidhiwa katika mamlaka ya wilaya ili yagawiwe kwa wananchi.
Kwa upande wa MPLC yenyewe inawaonesha washiriki hawa kazi zao katika eneo la Matombo ambako huko pia MPLC inafanya kazi za utetezi wa haki za umiliki wa ardhi kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto hiyo. Shirika hilo limejizolea sifa kwa kazi zake mkoani Morogoro na pia ni shirika kongwe ambalo linafanya kazi za utetezi na ushawishi mkoani Morogoro.
Washiriki kutoka Zanzibar wanatumia nafasi hii kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakumba makundi mbalimbali katika jamii ilhali kukiwa na mapungufu katika sera na maamuzi hali inahyowahitaji wananchi kufanya ushawishi na utetezi wa haki za kila kundi ili kuchochea jamii kubaki ikiishi kwa mani na ikiendesha maisha kwa mafanikio.
 Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Zainab Kisegele, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Ally Omary, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Washiri wakisikiliza kwa umakini
 Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Msowelo
 Washiriki waliokuwa wakielekea Matombo wakiwa katika gari kuelekea katika mafunzo kwa vitendo.


 Wakiwa katika mafunzo
 Wakiuliza maswali kwa wenyeji wao ili kujifunza zaidi
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
Ushuhuda .......
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Matombo.
 Baada ya mafunzo kwa pande zote mbili Msowelo na Matombo, washiriki walikutana tena na kuungana kwa majadiliano baada ya mafunzo kwa vitendo.



 
Washiriki wakijielezea jinsi walivyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao walokokwenda.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...