Thursday, April 28, 2016

Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo, akifunga rasmi Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) leo jijini Dar es Salaam.  

Mwenyekiti wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Geofrey Semu akizungumza katika mkutano wa THERIA leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioshirikisha wanachama wa THERIA kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania umefanyika kwa siku mbili mfululizo, Aprili 27 na 28, 2016 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili.

Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wake kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa THERIA uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akimkabidhi cheti cha shukrani mmoja wa wanachama waanzilishi wa THERIA kwa kufanikisha mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akikabidhi cheti cha shukrani kwa baadhi ya wanachama waliojitoa kufanikisha mkutano wa THERIA.


Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.
  
Sehemu ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (hayupo pichani) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja kati ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (katikati mwenye suti ya kijivu) pamoja na viongozi wa chama hicho na wageni wengine waalikwa.

Picha ya pamoja kati ya meza kuu, mgeni rasmi na viongozi na kamati ya mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...