Wednesday, April 13, 2016

Maswali na Majibu Kuhudsu Google Adsense



Malipo ya Google Adsense
Maswali na Majibu Kuhudsu Google Adsense


> MIMI ni mtumiaji wa google adsense kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita
> au zaidi , kupitia adsense nimeweza kupata kipato cha kuendesha maisha
> yangu kwa njia mbalimbali , kama ujenzi wa nyumba na uendeshaji wa
> biashara nyingine kupitia kipato hicho tu .
>
> Watu wengi wanapenda kujiunga na adsense na wengine walijiunga
> wakakata tamaa au hata wengine akaunti zao kufungiwa kutokana na
> kukiuka masharti kadhaa ya google adsense , mimi mwenyewe nilifungiwa
> mara 3 hivi na nilipoteza zaidi ya milioni 5 za kitanzania .
>
> Hili ni somo fupi kwa wale wanaopenda kujiunga na adsense au ambao
> wameshajiunga lakini wanataka kupata faida zaidi .
>
> Google Adsense ni nini ?
> Google adsense ni mfumo wa matangazo wa Google ambao unamwezesha mtu
> kitangaza bidhaa zake kwa kipato alichotacho na kumwezesha mwenye
> tovuti au blogu kufaidika kutokana na matangazo ya adsense kuonekana
> kwenye blogu yake au tovuti yake .
>
> Kwa lugha rahisi tunaweza kuita ppc Pay Per Click , Lipa kwa Click au
> mguso mmoja kwenye tangazo husika , mimi mwenye blogu hela utakuja
> kwangu kama mtu aligusa au gonga tangazo alilioona kwenye blogu yangu
> na yule aliyetangaza bidhaa zake kwenye google hela ndio inakatwa
> kutokana na click hiyo .
>
> Mimi nina blogu nyingi ambazo nimejisajili na google adsense ,
> ukiingia kwenye blogu hizo utaona matangazo yanaonekana yale matangazo
> sijaweka mimi na sijuani na walioweka matangazo hayo mimi yangu ni
> blogu na nafasi ya kutangaza niliyoiweka kwenye blogu .
>
> Unajiungaje na Adsense ?
>
> Adsense ni mali ya Google ni lazima au vizuri uwe na barua pepe ya
> gmail ambayo ni ya google au nyingine ambayo itakuwezesha kuweza
> kusajili adsense kwa urahisi lakini ni vizuri iwe imesajiliwa google .
>
> Usajili unakuwaje ?
> Tembelea 
www.google.com/adsense ukishasajili inachukuwa siku 15 kwa
> tovuti yako au blogu yako kuangaliwa kama inakidhi viwango vya google
> adsense kama lugha ,picha ,maudhui ,rangi na copyrights .
>
> Unaposajili unapewa CODE maalumu ambazo unaweza kuweka kwenye kurasa
> za tovuti au blogu yako kwa ajili ya kuanza kuonyesha matangazo
> mbalimbali .
>
> Nikisema lugha nina maanisha utumie lugha zinazokubalika na adsense
> kama kiingereza , kifaransa na nyingine za kimataifa Kiswahili
> hakitakiwi labda uchanganye ,kama blogu au tovuti yako ina picha chafu
> haitakiwi , rangi zake ziwe nzuri zisiingilie maslahi ya matangazo ya
> adsense na angalia milki ya vile unavyoweka .
>
> Baada ya siku 15 inakuwaje ?
>
> Baada ya siku 15 utapata email kama umekubaliwa au umekataliwa kama
> imekataliwa unaweza kuangalia ulichokosea na kubalisha kwa kukata
> rufaa unatakiwa ujaze appeal form ambayo nayo itaangaliwa kwa siku
> 15 .
>
> Kama umekubaliwa basi unatakiwa kuingiza dola 100 au euro 70 , hela
> hizi zinapatikana kutokana na matangazo yanayoonekana kwenye blogu au
> tovuti yako , ukiwa na kipato hicho utatumiwa kadi yenye namba ya siri
> ambayo utaingiza kwenye akaunti yako ili uweze kukamilisha usajili
> wako wa adsense , mlolongo huu unaweza kuchukuwa miezi 2 hivi .
>
> Unalipwaje ?
>
> Inategemea umechagua mfumo gani wa kulipwa , kuna mifumo 3 hivi
> inayojulikana zaidi .
>
> a)    Cheki – njia hii ilikuwa inatumika zaidi zamani hata sasa hivi kwa
> baadhi ya nchi na wale wanaopenda , kwa wale wa afrika inachukuwa siku
> 7 kupata cheki yako hapo utakatwa euro 17 kwa ajili ya kusafirisha
> cheki hiyo ,halafu unatakiwa kuingiza cheki kwenye akaunti yako ya
> benki ambapo inachukuwa siku 21 kulipwa au zaidi ya hapo – benki
> nyingine hazikubali cheki hizi kwahiyo wanaweza kukataa , kama
> ikikubali benki itakata hela ya kuprocess cheki .
>
> b)    Uhamisho wa Benki – Njia hii pia ni nzuri lakini kuna hela Fulani
> unakatwa kwa ajili ya kuhamisha hela kutoka nchi moja kwenda nyingine
> kwa njia ya benki na sio benki zote zenye huduma hii na inategemeana
> na kiwango cha hela inayotumwa kama ni ndogo sana inaweza kuwa tabu
> kidogo .
>
> c)    Western union – Hii ndio bora na ya haraka zaidi mara nyingi
> inalipwa kila mwisho wa mwezi unaofuatia kama ulipata dola 600 mwezi
> wa 3 utalipwa mwezi wa 4 mwishoni baada ya mahesabu kukamilika na
> baada ya kukatwa kodi na masuala mengine muhimu .
>
> NINI KISICHOTAKIWA ?
>
> 1 – Huduma nyingine za Matangazo , Kwa sababu adsense ni Pay Per Click
> ni bora usiweke matangazo mengine ya PPC kwa sababu yataingiliana na
> maslahi ya adsense unaweza kufungiwa au kuweka huduma nyingine za
> matangazo ambazo zinaweza kuzorotesha huduma za matangazo ya adsense .
>
> 2 – Kulazimisha watu kugonga au click au wewe mwenyewe kufanya hivyo ,
> hutakiwi kulazimisha watu kugonga matangazo ili ujiongezee
> kipato ,waache waangalie na kuamua wenyewe , kazi yako iwe ni kuweka
> taarifa za kutosha kwenye blogu au tovuti yako zinazovutia watu
> kutembelea na kuvutia watu wa masoko kupitisha matangazo yao kwenye
> kurasa zako .
> Hiyo namba moja ndio ya kwanza na muhimu zaidi nyingine ni Lugha ,
> haki miliki , picha chafu na rangi nzuri kwenye kurasa zako ambazo
> zitafanya matangazo kuonekana vizuri .
>
> FAIDA KWA MWENYE BLOGU TOVUTI
> Kutegemeana na aina ya blogu yako na maudhui lakini blogu au tovuti
> ili iweze kupata zaidi ya dola 15 kwa siku inatakiwa angalau kuwa na
> watembeleaji wa siku moja zaidi ya alfu 3000 , wanaotembelea toka nchi
> zinazoendelea na kuclick toka nchi za ulaya ndio wenye fedha na
> kuwezesha kulipwa vizuri zaidi kuliko nchi za afrika .
>
> Kwa Tanzania blogu ya kawaida yenye watembeleaji kati ya 2000 au 4000
> kwa Tanzania inatakiwa iwe na shilingi laki 9 kwa mwezi mmoja au zaidi
> kama kipato chake
>
> FAIDA KWA WATANGAZAJI /WAFANYABIASHARA.
> Utangazaji kwa kupitia adsense ni rahisi na fedha yako inaenda
> kihalali na ni rahisi kutokana na bajeti yako kama umepanga kutangaza
> kwa laki 1 kwa mwezi na unataka tangazo lako lionekane Tanzania pekee
> basi kwa kupitia adsense hiyo inawezekana kama unataka lionekana kwa
> lugha ya kiingereza pekee na lionekane japan au korea hilo
> linawezekana ni wewe kuamua na kufanikisha hilo kupitia adsense .
>
> Kama wewe ni mfanyabiashara huhitaji kuhangaika kutafuta blogu au
> tovuti kubwa kutangaza bidhaa zako ambako inaweza kuwa gharama zaidi
> na kupata nafasi ni finyu , fikiria adsense ifanyie kazi .
>
> ADSENSE INAWEZA KUWA AJIRA TOSHA ?
> Inategemea na mipango yako lakini adsense sio ya kuitegemea sana kama
> usipofuata taratibu unaweza kufungiwa lakini kama ukifuata masharti na
> kukaa nayo vizuri inaweza kuwa ajira yako inayokulipa vizuri na
> kufanya maisha yako kwenda vizuri .
>
> ADSENSE SIKU ZIJAZO .
> Sasa hivi watu wanatumia simu za mikononi na vifaa vingine kwa ajili
> ya kutembelea tovuti na blogu sio komputa kama zamani , kama ni
> mtumiaji wa adsense jiandae kwa hilo hakikisha matangazo yako ni
> mepesi na yanaweza kuonekana au kusomeka na watu wanaotuvmia vifaa
> hivi na kukulipa vizuri bila usumbufu mwingine .
>
> Kama unapenda kujua zaidi kuhusu adsense na msaada zaidi unaweza
> kunipigia kwa +255786806028 kama sipatikani andika sms kama uko Dar es
> salaam au Nairobi au Juba ni rahisi kuonana tunaweza kusaidiana .
>
Imeandaliwa na Yona F Maro

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...