MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI
YA DARAJA LA KIGAMBONI
WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la
kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia
saa 12:00 asubuhi.
Katika
siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali
itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia. Aidha, watembea kwa miguu na waendesha
baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni. Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa
kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.
Magari
yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo
ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo
wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo
la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika
daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela,
Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.
Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito
unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo
muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia
ni:-
1)
Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na
kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu
miundombinu ya daraja
2)
Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’
ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3)
Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo
cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo
hicho.
4)
Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha
uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au
kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5)
Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la
daraja.
Aidha,
Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo
wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini
watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano
wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa
watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Imetolewa
na;
Eng.
Joseph M. Nyamhanga
Katibu
Mkuu (Ujenzi)
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14
Aprili, 2016
No comments:
Post a Comment