Tuesday, December 4, 2012

Harusi ya Mjuni Makubo na Mkewe Dorothea Mjuni


Bwana Harusi Mjuni Makubo akiwa katika picha ya Pamoja na Baadhi ya Wapambe wao katika sherehe ya harusi yao iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Desemba Mosi 2012.
  Bwana Harusi Mjuni Makubo Pamoja na Mkewe wakiwa katika Picha ya Pamoja na Ndugu zake Kabla ya kuingia Ukumbini. Kutoka Kushoto ni Mugisha Msheluzi Makubo akifuatiwa na Mkewe Diana, Mdogo wa Bwana Harusi Fiona Makubo, Mjuni na Mkewe, Akifutiwa na Mdogo wake bwana Harusi Leoncia Makubo, Mama yake Mjuni Makubo Bi Lydia Makubo na Mdogo wake Lukiza Makubo 
 
  Mr Na Mrs Mujuni Makubo wakiwa katika pozi mara baada ya kuingia ukumbini katika sherehe fuppi ya Ndoa yao iliyofanyika Katika Ukumbi wa Mlimani City Desemba Mosi 2012.
 
 Bibi Na Babu yake Mjuni Makubo, Mama Leoncia Lukaza na Justus Kato Lukaza (wazazi wa baba Mjuni Mzee Makubo) wakitoa neno kwa wajukuu zao Dorothea na Mjuni Makubo katika hafla ya harusi yao iliyofanyika Desemba Mosi 2012 katika Ukumbi wa Mlimani City.
  Baba wadogo Wa Bwana Harusi Mjuni Makubo.Kutoka Kushoto Ni Mgisha Lukaza, Katikati ni Bwana Harusi Mwenyewe Mjuni Makubo na Mwisho ni Mwesigwa Lukaza wakiwa na nyuso za furaha baada ya kijana wao kuaga rasmi maisha ya ukapera.
 
 Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya harusi ya Mjuni na Dorothea Makubo iliyofanyika Katika Ukumbi wa Mlimani City Desemba Mosi 2012.
 
Hii ndio Kamati Nzima ya Maandalizi ya Sherehe ya Harusi ya Mjuni na Dorothea Makubo iliyofanyika Desemba Mosi 2012 katika Ukumbi wa Mlimani City.
 
 Baba Mzazi na Mama Wa Bwana Harusi Mh Mjuni Makubo wakitoa nasaha kwa watoto wao mara baada ya kufunga ndoa takatifu na sherehe fupi kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City Desemba Mosi 2012.
 
 Wazazi wa Bibi Harusi wakitoa Nasaha kwa Watoto wao mara baada ya kufunga ndoa takatifu na sherehe kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City Desemba Mosi 2012.
 
Kwa Mila za Kihaya Mwanaume anapooa Wazazi wake umkabidhi Mkuki Kwa ajili ya Ulinzi na Sio Kumdhuru na Kumpiga Mkewe.
 
Mzee Makubo (Baba Mzazi ) wa Bwana Harusi Mjuni Makubo Akimvalisha Kanzu ikiwa kama ishara na Mila za kihaya kwamba Ameshakuwa na anaweza Kuchangia katika Vikao vya Watu wazima
 Bwana na Bibi Harusi Mjuni Na Dorothea Makubo wwakisubiri kukata keki tayari kwa kulishana ikiwa ni ishara ya Upendo katika Ndoa yao.   

 
 Zawadi kutoka Kwa ndugu jamaa na marafiki.
  Baba Mdogo wa Bwana Harusi Jonnes Lukaza akifuatilia kwa makini kila Kinachoendelea katika Ukumbi huo.  Picha kwa hisani ya Blog Lukaza.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...