Wednesday, June 1, 2016

USAID wahaidi kuendelea kuisaidia miradi anuai Tanzania




Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya serikali ya Marekani katika mkutano wa hitimisho wa mradi wa SCMS.

Na Rabi Hume, Dar

BAADA ya mradi wa SCMS kufanyika nchini kwa miaka 10, huku ukisimamiwa na taasisi ya John Snow Incorporated (JSI) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) limeiahidi serikali ya Tanzania kuwa litaendelea kuisaidia katika misaada mbalimbali ya afya licha ya kumalizika kwa mradi huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay katika mkutano ambao ulikutanisha wadau mbalimbali wa afya ili kujadili mradi wa SCMS ambao umefikia tamati baada ya kufanyika nchini kwa miaka 10.

Bi. Donnay alisema serikali ya Marekani kupitia USAID imejipanga kuendelea kuisaidia Tanzania katika sehemu mbalimbali ambazo zinahusu Afya.

“USAID itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya upatikanaji wa huduma bora wa kiafya ... kumalizika kwa mradi huu hukutafanya kusitishwa kwa huduma ambazo zinatolewa kwa sasa,” alisema Bi. Donnay.

Naye mgeni rasmi katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Mpoki Ulisubya alisema kufanyika kwa mradi huo nchini kumewezesha kusaidia kuboreshwa kwa kasi huduma za afya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Mradi huu umetusaidia sana awali hata utolewaji wa dawa kwa waathirika wa UKIMWI ulikuwa ni laki na nusu kwa mwaka ila kwa sasa kuna upatikanaji wa dawa hadi laki nane kwa mwaka,

“Mbali na hiyo pia wametujengea maghala ambayo yanatumika kuhifadhi dawa na hata kusaidia kuweza kuwasogezea huduma wananchi ambazo awali hazikuwa zikitolewa,” alisema Ulibusya.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...