Sunday, June 12, 2016

NSSF Yawaandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma...!

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea na Madereva wa Bodaboda (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa rasmi wa Kampeni ya Kuandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya semina na kuzindua mpango wa kuwaandikisha maadereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma, Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA , Trafiki Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.

Pamoja na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama aliwapatia Vifaa vya Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo ni Kofia ya Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua mfumo wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda mkoani Dodoma.


Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu kwa Madereva wa Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa kampeni rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.

Waziri akikabidhi moja ya pikipiki ambazo wamekopeshwa madereva wa Bodaboda Dodoma na Manispaa ya Dodoma. Wakishuhudia ni Mwakilishi wa Kamanda wa Trafiiki Mkoa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvalisha mmoja wa Madereva wa Bodaboda Kofia Ngumu ya Usalama iliyotolewa na NSSF. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof, Godius Kahyarara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvesha Jaketi maalumu la Usalama Dereva wa Bodaboda Mkoa Dodoma akimsaidia Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa Kituo Cha Bodaboda kwa Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoani Dodoma Bang'ara Lucas Kang'alo akishuhudia katikati Mkurugenzi wa NSSF Prof Godius Kahyarara.

Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Kazi, Ajira, Vijana na  Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa Bahi Francis Mwonga( Wa Kwanza kulia kwa Waziri), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (Kushoto kwa Waziri) na Mkuu wa Chuo cha Veta Dodoma Bw. Mattaka baada ya kupokea mfano wa kadi ya Mwanachama ya NSSF akiwa mmoja ya wanachama wapya waliojiunga NSSF.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...