Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa (kushoto) na Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za malipo ya Star Times kupitia benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi.
Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa (kulia) na Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kushoto) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za malipo ya Star Times kupitia benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kushoto) akitoa ufafanuzi namna mteja wao anaweza kufanya malipo kupitia benki ya NMB. Kulia ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa akifuatilia.
Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa (kulia) na Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kushoto) wakipongezana mara baada ya kuzinduwa rasmi huduma za malipo ya Star Times kupitia benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
BENKI ya NMB Tanzania imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Star Times ambapo kwa sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi.
Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za Star Times, ambapo Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa alisema wateja wa NMB waliounganishwa na huduma za kibenki kwa simu za mkononi sasa watafanya malipo yao popote walipo na kwa urahisi, huku wateja wa Star Times ambao hawana akaunti na benki hiyo kuweza kulipia huduma katika tawi lolote la Benki ya NMB.
Alisema huduma hiyo licha ya kuwarahisishia kazi wateja itakuwa haina tozo kwa wateja wa NMB hivyo kuwataka wananchi na wateja wa Benki ya NMB waitumie ipasavyo. Alisema hatua ya Benki ya NMB yenye zaidi ya wateja milioni mbili Tanzania huku ikiwa na matawi zaidi ya 176 itasogeza zaidi huduma za malipo ya ving'amuzi vya Star Times kwa wateja mbalimbali.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa NMB, Bwana Damien alisema wateja wa NMB na wengine wasio na akaunti watakapoitaji huduma ya malipo watatakiwa kubofya *150*66# na kuchagua huduma ya malipo ya Star Times na kuendelea kupata maelekezo rahisi katika kufanikisha malipo yao.
Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Wednesday, June 29, 2016
Sunday, June 26, 2016
Naibu Spika Dk Tulia Aosha Magari ya Wabunge, Mawaziri Kuwaunga Mkono Wanahabari
Mmoja wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
Mmoja wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
Saturday, June 25, 2016
Friday, June 24, 2016
Regnald Mengi Achangia Madawati 1,000
KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.
Hata hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa kusuasua.
"Ukisaidia mtu mmoja katika elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.
"Matajiri wanatakiwa kutambua kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya biashara zao kwa amani," alisema Dk. Mengi.
Aidha amewataka wakuu wa wilaya hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.
Kwa upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk. Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.
Awali kabla ya msaada ambao umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati 4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza tatizo la madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu.
Thursday, June 23, 2016
Ubia wa TTCL na Bharti Airtel Wafikia Kikomo
Tuesday, June 21, 2016
Mchezo wa Shuga wabadilisha tabia za vijana Iringa na Mbeya
Mratibu wa mradi wa Shuga akijibu maswali yaliyokua yanaulizwa na kikundi cha wasikilizaji cha Iwawa- Makete mkoani Njombe
|
Wakionyesha furaha zao baada ya kuelewa mada ya siku ukihusianisha na maisha yao ya kila siku |
Mwezeshaji wa kikundi cha wasikilizaji wa Kihesa, Manispaa ya Iringa mjini akitimiza jukumu lake la kuelimisha wenzake na kuwawezesha kushiriki katika majadiliano baada ya kusikiliza kipindi |
Vijana wa Iringa wakionyesha nyuso zenye furaha baada ya kuongeza uelewa kupitia majadiliano baada ya kipindi cha saba cha mfululizo wa vipindi vya Shuga
|
Kikundi cha wasikilizaji kutoka kijiji cha Kabanga, Kyela wakifurahia uelewa walioupata juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika maisha yao
|
Kikundi cha wasikilizaji Jitambue 1 kutoka wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wakijadiliana sehemu ya saba ya mfululizo wa vipindi vya mchezo wa redio wa Shuga. |
Wakina mama wakifuatilia mjadala kuhusu kujitambua na namna ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI pamoja
|
Mwana kikundi wa AMKA- Njombe vijijini akiwashirikisha wanakikundi wenzie uzoefu wake katika kukabiliana na changamoto za kutakwa kimapenzi na wanaume waliomzidi umri |
Tunajitambua, Tunajipenda na Tunajilinda na VVU. Tumepima - Kikundi cha AMKA kutoka Njombe
|
UGONJWA wa UKIMWI umekuwa janga kubwa sana duniani huku wadau mbalimbali wakiendelea kutoa elimu na kuhamasisha katika kuanzisha programu mbalimbali za kubadilisha tabia chanya kwa jamii.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Mratibu wa mchezo wa redio wa Shuga alisema tayari wameanzisha programu mbalimbali za vipindi vinavyolenga kuelimisha jamii hususani vijana juu ya maambukizi ya Virusi vya ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI), usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kinga na kuepukana na msongo rika.
Alisema mfululizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio pamoja na changamoto wanazopitia kwa njia sahihi za kukabiliana na changamoto ili kutimiza malengo yao.
"Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga," alisema Laizer
Alisema mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga awamu ya pili vilianza kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne 2016 kwa lengo la kuendeleza elimu ya masula ya UKIMWI.
"Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na maudhui ya vipindi, kampuni ya True Vision Production imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa awamu ya pili ya mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya masuala hayo." alisema Laizer. "Kwa sasa, vituo mbalimbali vya redio vinarusha sehemu ya nane ya mfululizo wa vipindi vya Shuga." Aliongezea Laizer.
Alisema Matokeo ya mradi huu yameanza kuonekana na vijana ambao ni walengwa wakuu wametoa ushuhuda wao kuhusiana na kipindi hicho cha Shuga na kusema kuwa klipindi kimewaletea mabadiliko makubwa.
‘Vijana tunajitambua, tumehamasika kwenda kupima afya zetu, tunajua njia sahihi za kujilinda na magonjwa ya zinaa na pia tunajiwekea mipango endelevu," alisema Abbas Boniphace, mmoja wa wasikilizaji wa kipindi cha Shuga kutoka Njombe
"Ningepata nafasi ya kusikia Shuga mapema nisingepata ujauzito katika umri mdogo. Sikua na uelewa wakati huo, sasa najitambua, nimepima na najilinda, siwezi kudanganyika" alisema Herieth kutoka Njombe.
"Wazazi huogopa kutuambia ukweli juu ya maswala yahusuyo VVU na UKIMWI ila Shuga inaelezea kwa uwazi zaidi." Alisema Shamila Juma, mwana kikundi cha wasikilizaji wa vipindi vya Shuga
Muhubiri Masanja Mkandamizaji Atinga Mkutano wa OYES 2016 Mwanza...!
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Thursday, June 16, 2016
DC Ataka Watoto Ombaomba Mwanza Waondoshwe...!
Halleluyah Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza, akisima risala ya watoto katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika hii leo. |
Watoto kutoka taasisi ya "Pamoja Youth and Children Foundatio" ya jijini Mwanza wakionyesha michezo ya sarakasi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Halmashauri ya Jiji la
Mwanza kwa kushirikiana na idara ya Ustawi wa Jamii, imetakiwa kuwaondoa watoto
waliozagaa mitaani ambao wamekuwa wakiomba misaada kwa wasamaria barabarani.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku
ya Mtoto wa Afrika ambayo kwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza yamefanyika shule ya msingi
Mabatini, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, amesema wengi wa watoto hao
wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufiwa na wazazi ama
wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kimasomo, hivyo Halamshauri hiyo ina
wajibu wa kuwasaidia.
Amesema hatua ya kuwaondoa watoto hao
inaweza kuonekana ni ngumu kutekelezeka, lakini inawezekana ikiwa kila mdau
ikiwemo jamii itatoa ushirikiano ambapo amewasihi madiwani katika baraza la halmashauri ya Jijini la Mwanza kupeleka hoja
kwenye baraza lao ili jambo hilo liwekwe kwenye vipaumbele vya Halmashauri hiyo.
"Mkurugenzi, Meya na Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza, chukueni hatua kuwaondoa watoto waliozagaa mitaani ikiwemo mtaa wa Nkuruma kwani hawako pale kwa kupenda. Mkifanya hivyo itakuwa sifa kwenu na kwa baraza la madiwani la mwaka 205/20". Amesema Konisaga.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka June,16 ikiwa ni kumbukumbu ya mauaji ya mamia ya watoto waliouawa na polisi wa kikaburu mwaka 1976 katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini wakati walipokua wakiandamana kupinga kubaguliwa kielimu kwa kufundishwa katika lugha wasiyoifahamu ya Afrikana.
Katika risala yao, watoto wameiomba serikali pamoja na jamii kuwalinda na vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ukatili unaowakumba ikiwemo kukosa elimu.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga (wa kwanza kushoto), ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, akizungumza katika maadhimisho hayo.
Halleluyah Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza (kushoto) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Paulina Robert.
Wanafunzi wakisoma ngojera katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
Mshereheshaji kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza
Wahudhuriaji akiwemo mtoto kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza, wakiendelea kufuatilia maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga (wa tatu kushoto), wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
Subscribe to:
Posts (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...
-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo ...