Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi
(MUWSA) Joyce Msiru ,akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Gerson Lwenge juu ya mradi wa chanzo cha
maji cha Kisimeni
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi MUWSA,Mhandisi Paatrick Kibasa akimueleza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Geryson Lwenge namna ambavyo maji yanayopatikana katika chemichemi ya Kisimeni yanavyotibiwa kabla ya kwenda kwa mtumiaji wa mwisho.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika mradi wa Chemichemi ya Kisimeni kwa ajili ya uzinduzi.anayeshuhudia ni mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akiondosha kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa Maji wa chanzo cha maji cha Chemichemi ya Kisimeni.
Vijana wa Skauti wakimvisha Skafu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Lwenge alipowasili uwanjani hapo.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Prof Faustine Bee akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Joyce Msiru akitoa taarifa ya mamlaka hiyo kwa Mh,Waziri wa maji na umwagiliaji ,Mhandisi Geryson Lwenge pamoja na taarifa ya mradi wa maji ya Chemichemi ya Kisimeni ambao umetekelezwa ndani ya siku 100.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Geryson Lwenge akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji yanayotokana na Chemichemi ya Kisimeni.
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Longuo wakitoa burudani ya wimbo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Kisimeni.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akizindua rasmi mradi wa maji katika kata Uru kaskazini.
Waziri Lwenge akimbebesha ndoo mmoja wa wakazi wa Longuo mara baada ya kufanya uzinduzi wa mradi huo.
Mgeni rasi katika uzinduzi huo ,Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Geryson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi,mameneja wa mamlaka hiyo na viongozi wengine waliofika katika uzinduzi huo.
Wakuu wa wilaya ,Anhtony Mtaka,(wilaya ya Hai) Novatus Makunga (wilaya ya Moshi mjini ) na Mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment