Thursday, February 11, 2016

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF

Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF. Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.[/caption]
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaju akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...