Saturday, November 7, 2015

JK Aondoka Rasmi Ikulu Kuelekea Kijijini Msoga Bagamoyo...!










Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuondoka rasmi Ikulu kabla ya kupanda chopa kuelekea kijijini Msoga Wilayani Bagamoyo kuanza rasmi mapumziko ya kustaafu wadhifa wake.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. Kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
  Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
  Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga
 Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho kikwete

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...