|
Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akionesha mkuki na ngao kama ishara ya mamlaka mara baada ya kula kiapo leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. |
|
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. |
|
Jopo la majaji wa Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu, Othman Chande (hayupo pichani) wakielekea jukwaa la kiapo, ambapo Jaji Mkuu alimuapisha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Baadhi ya maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Wageni mbalimbali walioshiriki sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Wananchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Wananchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kula kiapo kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano. |
|
Rais mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (kushoto) na Makamu wake, Dk. Gharib Bilal (kulia) wakiaga wananchi mara baada ya kumaliza awamu yao. |
|
Bendera ya Rais wa Tanzania ikipandishwa ikiashiria kuanza kwa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Dk. Magufuli. |
|
Baadhi ya marais wa nchi mbalimbali na viongozi wakuu wa nchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais Dk. John Magufuli. |
|
Baadhi ya maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama wakitoa saluti kwa wimbo wa taifa leo... |
|
Uwanjani sherehe za kiapo cha rais na makamu wake. |
|
Gwaride...Kikosi cha bendera kikitoa heshima kwa rais kwenye sherehe za kiapo cha Rais na Makamu wake. |
|
Wageni waalikwa kwenye sherehe za kiapo cha Rais wa Tanzania na Makamu wake. |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo ameapishwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015. Dk. Magufuli amekula kiapo hicho leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru pamoja na Makamu wake wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiahidi kulitumikia taifa kwa uaminifu, unyenyekevu bila ubaguzi wowote.
Sherehe za kuapishwa kwa Rais Dk. Magufuli na Makamu Rais wake, Mama Suluhu Hassan zimehudhuriwa na marais wa nchi mbalimbali, viongozi wawakilishi kutoka mataifa anuai, mabalozi, viongozi wastaafu wa Serikali ya Tanzania, maofisa wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, wabunge wateule na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Miongoni mwa marais walioshiriki katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Congo (DRC), Joseph Kabila, Rais wa Zimbabwe, Robart Mugabe, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na viongozi wengine wengi kutoka mataifa mbalimbali.
Aidha, Dk. Magufuli amekabidhiwa kijiti na Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ambaye anakwenda kupumzika baada ya kulitumikia taifa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano alivyochaguliwa kuliendesha taifa la Tanzania. Licha ya uwepo wa mvua jijini Dar es Salaam tangu alfajiri ya leo sherehe za kiapo cha Dk. Magufuli zimehudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi walioanza kuingia uwanjani tangu saa kumi na moja ya asubuhi. Uwanja wa Uhuru ulifurika hivyo kuamriwa wananchi kuanza kuingia katika Uwanja wa Taifa ambao ulikuwa ukionesha matukio ya kiapo kupitia runinga kubwa zilizofungwa katika uwanja huo ambao nao ulifurika.
Watanzania wanamatumaini makubwa na Rais Dk. Magufuli kutokana na historia ya utendaji katika baadhi ya nafasi za uwaziri alioshika hapo nyuma, ambapo amekuwa akifanya vizuri kiutendaji kiasi cha kumpa jina la utani la 'Tingatinga' jina lililoendelea kuvuma hadi sasa. Tanzania inaingia katika historia ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni nafasi ya juu ya uongozi wa nchi kushikwa na mwanamama tangu nchi ipate uhuru wake.
No comments:
Post a Comment