Thursday, July 5, 2012

Harusi ya Oltesh Eliguard na Ssanyu Sylvia jiji Dar

 
 Maharusi, Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali waliofika ndani ya Kanisa la Azania Front, mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu, katika kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu, Dk. Alex Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya maharusi hao kuvishana.



Maharusi wakilishana kiapo cha ndoa mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliofika kanisani hapo mapema leo mchana kuishuhudia ndoa hiyo ya Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi, iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania Front.
 
 Maharusi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja mapema leo ndani ya Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Pichani kushoto ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakishuhudia pia tukio hilo adhimu na la kihistoria kwa Wanandoa.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...