Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina alipokutana nayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni | Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour. | |
Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (wa kwanza kushoto) kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea. |
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo (kushoto) akitoa utaratibu wa mazungumzo katika mkutano huo na wanahabari. |
No comments:
Post a Comment