Wednesday, January 18, 2017

Makosa ya watumiaji barabara yanavyoatarisha maisha ya watumiaji wengine

Eneo hili ni kivuko cha waenda kwa miguu kilichomo borabara ya Mandela jijini Dar es Salaam. Pichani waenda kwa miguu wanavuka japo kuna magari ambayo yameingia ndani ya hifadhi ya kivuko hicho kimakosa. Watumiaji wengi wa barabara wamekuwa wakijisahau katika maeneo haya. 



Wakati mwingine waenda kwa miguu hulazimika kuvuka wakati magari yakipita eneo la kivuko, kwa kile watumiaji wengi wa barabara hasa madereva kutotoa kipaumbele katika maeneo hayo. Pichani mwananchi akivuka moja ya kivuko kilichomo borabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.


Wakati mwingine waenda kwa miguu husubiri kwa muda mrefu kabla ya hulazimika kuvuka wakati magari yakitembea eneo la kivuko, kwa kile watumiaji wengi wa barabara hasa madereva kutotoa kipaumbele katika maeneo hayo. Pichani wananchi wakisubiri kuvuka moja ya kivuko kilichomo borabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.



Wakati mwingine waenda kwa miguu hulazimika kuvuka huku wakikimbia katika eneo la kivuko kana kwamba hawaruhusiwi kwa kile madereva wengi kutotoa kipaumbele katika maeneo hayo. Pichani mwananchi akivuka huku akikimbia katika moja ya kivuko kilichomo borabara ya Mandela jijini Dar es Salaam.



Na hapa watumiaji wa kivuko cha waenda kwa miguu wakivuka kwa kukimbia eneo la kivuko kwa kile madereva wengi kutotoa kipaumbele katika maeneo hayo.



Moja ya gari likiwa limesimama katika voleni na kuziba kivuko cha waenda kwa miguu, huku mtumiaji wa kivuko akiwa amesimama katikati ya kivuko hicho kwa kushindwa kuvuka.



Watumiaji wengi wa vyombo vya moto barabarani hukiuka sheria ya usalama barabarani hasa kwenye vuvuko vya waenda kwa miguu. Pichani ni bodaboda na abiria wake wakitumia kivuko cha waenda kwa miguu kinyume na sheria.

Baadhi ya wananchi na abiria wa daladala linalofanya safari zake Mwenge Posta wakilisukuma gari lililogongana na kuacha njia. Kwa mujibu wa mashuhuda gari hili lililokuwa likitanua kabla ya kuingia barabarani gafla na kusababisha ajali Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.


Mwendesha bodaboda pamoja na abiria wake akitumia barabara eneo lisilo sahihi jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wengine. Pamoja na hayo dereva huyu na abiria wake hawajavaa kofia ngumu jambo ambalo ni kosa lingine kisheria.

Mwendesha bodaboda pamoja na abiria wake wakiwa barabarani na kuvunja sheria kwa kile kutovaa kofia ngumu jambo ambalo ni kosa kisheria.


Kutokuzingatia sheria kunasababisha ajali kama hizi ambazo hupoteza maisha ya watu na mali na kufanya uharibifu. Pichani magari yakiwa yamegongana eneo la Tabata Segerea. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo gari la upande wa kushoto lilikuwa likitumia upande usio wake jambo ambalo ni makosa. 


Waendesha bodaboda wakiwa wameegesha bodaboda zao eneo la hifadhi ya barabara jambo ambalo ni hatari kwao. Pichani wakishauriwa kuondoka eneo hilo na mmoja wa maofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani eneo la Mbezi Standi Mpya. 


Waendesha bodaboda wakiwa wameegesha bodaboda zao eneo la hifadhi ya barabara jambo ambalo ni hatari kwao. Pichani wakishauriwa kuondoka eneo hilo na mmoja wa maofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani eneo la Mbezi Standi Mpya. 

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...