Tuesday, January 31, 2017

Halmashauri ya Monduli na Kashfa ya Ugawaji Ardhi, Wananchi Waja Juu

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli.




wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo





wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara






MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikiny






Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo


Habari/Picha na Woinde Shizza, Arusha

BADDHI ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao

Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao.

Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.

“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama wa CCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti

Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.

Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.

Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi.

“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu," alisema Sanare.

Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia. Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...