Tuesday, July 19, 2016

Benki ya NMB yaorodhesha Hati Fungani zake kwenye soko la hisa, DSE



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (katikati) akipiga kengele kuashiria kuorosheshwa rasmi hati fungani za Benki ya NMB kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kulia).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (katikati) akipiga makofi mara baada ya kuashiria kuorosheshwa rasmi hati fungani za Benki ya NMB kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kulia).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) mara baada ya tukio la Benki ya NMB kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi bilioni 41.4 katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). 

  BENKI ya NMB leo imeorodhesha kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 ilichokipata kutokana na mauzo ya hati fungani katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Tukio hilo limezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru kwa ishara ya kupiga kengele kwenye ofisi za DSM.

 Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Meru alipongeza hatua hiyo ya kuorodhesha hati fungani kwenye soko la hisa na kuongeza kuwa ni ya kizalendo na kuwataka wawekezaji katika sekta binafsi kushiriki kikamilifu.

 “Hati fungani hii inatarajiwa kuleta maendeleo katika soko la mitaji na inafungua njia kwa mashirika mengine binafsi, mashirika ya serikali na mamlaka za manispaa kutafuta njia mpya za kukuza mitaji na uwezeshaji” alisema Dk. Adelhelm.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NMB - Ineke Bussemaker alisema “Hati fungani hii ya miaka mitatu si tu imeleta msisimko chanya kwenye soko la mitaji bali hata katika soko la hisa, NMB inakuwa benki ya kwanza kupata Kiwango zaidi ya mara mbili ya Kiwango tulichoomba awali.” Bi Ineke.

Aliongeza kuwa mwitikio chanya kwenye hati fungani ya NMB unatoa somo kuwa kuna umuhimu wa benki mbalimbali kuchangia kwa Kiwango kikubwa katika kuendeleza masoko ya mitaji na pia kupigania elimu ya fedha kwa jamii. Hati fungani inayoorodheshwa leo ina riba ya asilimia 13 kwa mwaka na iitakomaa baada ya miaka miatatu. Bi Ineke alisema Kutolewa kwa hati fungani ya NMB ni sehemu ya mkakati wa benki kutafuta njia mbadala za vyanzo vya fedha.

Fedha zilizopatikana kwenye hati fungani zitatumika kwaajili ya kutoa mikopo kwa wateja, wateja watakaonufaika ni pamoja na wateja binafsi, wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na taasisi za serikali.

 Akiongea kwenye hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE - Moremi Marwa alisema “mafanikio ya Hati fungani ya NMB yanatuambia kuwa wawekezaji wanajua uwepo wa fursa zilizopo katika masoko ya mitaji na wana uwezo na hamu ya kusaidia wale walio na uhitaji wa kukuza mitaji yao.”

 Hati fungani ya NMB ilipata mwitikio chanya kutoka kwa wawekezaji na kupita Kiwango kilichopangwa awali kwa asilimia 107. Benki ilipata maombi 1,811 yenye thamani ya shilingi bilioni 41.4 huku maombi mengi yakirundikana wiki ya mwisho kabla ya kufunga upokeaji wa maombi.

Kutokana na kuorodheshwa kwenye soko la hisa, wawekezaji wataweza kuuza hati fungani zao kupitia soko la hisa la Dar es Salaam – DSE. Stanbic Bank Tanzania Ltd. Ndio wawezeshaji wa hati fungani ya NMB huku makampuni ya Orbit Securities Ltd. na EA Capital Ltd wakiwa kama mawakala viongozi.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...