JESHI LA
POLISI TANZANIA LINAWAJULISHA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO
CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI
KUWA WANATAKIWA
KURIPOTI KWA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA TAREHE 28/08/2015 KWA AJILI
YA MAANDALIZI YA USAFIRI WA KWENDA SHULE YA POLISI TANZANIA
TAREHE 29/08/2015.
KILA MMOJA ATATAKIWA KUWA NA NAULI
YA KUMWEZESHA KUSAFIRI TOKA MAKAO MAKUU YA MKOA ANAKOANZIA KUSAFIRI HADI SHULE
YA POLISI MOSHI NA ATAREJESHEWA NAULI ATAKAPOFIKA CHUONI BAADA YA KUWASILISHA
TIKETI YA SAFARI. AIDHA TAREHE YA MWISHO YA KURIPOTI CHUONI NI TAREHE 05/09/2015 NA ATAKAYERIPOTI BAADA YA
HAPO HATAPOKELEWA.
AIDHA VIJANA HAO WATALAZIMIKA
KUFIKA SHULENI WAKIWA NA VITU VIFUATAVYO :
1.VYETI VYAO
VYOTE VYA MASOMO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATES/RESULT SLIP PAMOJA NA LEAVING
CERTIFICATES) KIDATO CHA NNE, SITA NA VYUO.
2.VYETI
HALISI VYA KUZALIWA (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATES). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA
HAITAKUBALIKA.
3. MASHUKA
MAWILI RANGI YA BLUU BAHARI (LIGHT BLUE)
4.CHANDARUA
CHENYE UPANA FUTI TATU
5.NGUO ZA
MICHEZO (TRACK SUIT NYEUSI,T-SHIRT BLUE NA RABA)
6.PASI YA
MKAA.
7.NDOO MOJA.
8.PESA ZA
KULIPIA BIMA YA AFYA KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA MIA NNE TU (50,400/=).
9.PESA KIDOGO
YA KUJIKIMU.
ZINGATIA: KWA MUJIBU
WA KANUNI ZA SHULE YA POLISI NI MARUFUKU KUFIKA SHULENI NA SIMU YA MKONONI.
ATAKAYEPATIKANA NA SIMU ATAFUKUZWA SHULENI HAPO. SHULE ITAELEKEZA NA KUSAIDIA
KUFANYA MAWASILIANO.
MAJINA YA WAHITIMU YANAPATIKANA
KUPITIA TOVUTI www.policeforce.go.tz au WAFIKE
OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment