Monday, August 31, 2015

UKAWA WAZINDUA KAMPENI ZAO MOSHI



Baadhi ya viongozi na wagombea wa nafasi za Udiwani Kupitia Chadema na Ukawa.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Philemoni Ndesamburo(kushoto) akiteta jambo na  mgombea Ubunge katika jimbo hilo ,Jafary Michael kupitia Chadema na UKAWA wakati wa uzinduzi wa kampeni mjini Moshi

Umati wa wakazi wa mji wa Moshi waliofika katika mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni.



Mbunge wa Viti maalumu Chadema ,Lucy Owenya akizungumza katika mkutano huo.
Meneja wa kampeni wa mgombea ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Raymond Mboya akisalimia katika mkutano huo.  

Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema akitoa salamu za chama katika mkutano huo.


Umati wa wakazi wa Moshi katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburo akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Philemoni Ndesamburo akimtamburisha kwa wapiga kura ,mrithi wake katika kinyang'anyiro cha kuwania nafai ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael aliyekuwa Meya wa manispaa hiyo.


Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika mkutano huo.


Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akiomba kura mbele ya wapiga kura wakati wa uzunduzi wa kampeni katika jimbo la Moshi mjini.





Sunday, August 30, 2015

ACT-WAZALENDO Yazindua Kampeni zake Zakhem Mbagala

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini 
Dar es Salaam 
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.
 Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
  Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
 Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

UZINDUZI WA KIPINDI CHA MASHARIKI MAX

Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm akitoa hotuba ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times katika nchi za Afrika Mashariki wakati wa hafla ya uzinduzi huo  jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Group nchini Langtang Liao akimkaribisha Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm wakati wa hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times

Mtangazaji wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia Televisheni ya Star Times Jokate Mwegelo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Group nchini Langtang Liao

Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Group nchini Langtang Liao (wa tatu kulia) wakifuatilia uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia Televisheni ya Star Times wakati wa uzinduzi wa kipindi hicho jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia Televisheni ya Star Times

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia Televisheni ya Star Times

BOA Tanzania Yakusanya zaidi ya Milioni 210 Kusaidia Watoto Waliozaliwa na Miguu Iliyopinda

  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili  Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani  kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya CCBRT

NA  FRANCIS DANDE

RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana aliongoza  matembezi ya hisani ya kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya watoto waliopinda miguu.

Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika - Tanzania, lengo kuu lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa  ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika – Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli  zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata  matibabu,” alisema Mwanaidi .

Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza: “ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa  Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya  watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”

Tamasha la Kuombea Amani Uchaguzi Mkuu Kufanyika Oktoba 4,2015

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu  utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu  utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Benno Chilele (kushoto), akizungumza katika tamasha hilo. Kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa Tamasha la Krismas na Pasaka, Alex Msama. 
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com\

Lowassa; Nikiingia Ikulu Elimu ni Bure Mpaka Chuo Kikuu

Uzinduzi wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Jangwani jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Jangwani jijini Dar es Salaam.Uzinduzi wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Jangwani jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Jangwani jijini Dar es Salaam.[/caption]Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam WAKATI moto wa kampeni za Uchaguzi Mkuu ukipamba moto mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amekuja na ahadi ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Lowassa ametoa kauli hiyo akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Jangwani na kuhudhuriwa na maelfu ya wapenzi wa chama hicho pamoja na washirika wake. Chadema ambayo inaungwa mkono na vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na NLD katika uzinduzi huo imeeleza ilani yao kipaumbele cha kwanza hadi cha tatu ni elimu, kwani kinaamini Watanzania wakipata elimu bora safari ya maendeleo itakwenda haraka. Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alimkabidhi mgombea urais, Lowassa pamoja na mgombea mwenza ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuahidi itazungushwa takribani mikoa yote ikinadiwa. Hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni za urais kwa Chadema ambazo pia zinaungwa mkono na vyama vine kupitia umoja na ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA, iliohudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama hivyo, ulipambwa na jumbe za mabango mbalimbali yaliyokuwa yameshikwa na wananchi. Akifafanua zaidi mgombea, Lowassa baada ya kukabidhiwa ilani ya chama chake alisema vipaumbele katika ilani ya kuwa ni elimu, ambapo alieleza kuwa ili nchi iendelee ni lazima kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na serikali kugharamia elimu hiyo kutoka darasa la kwanza hadi chuo kikuu jambo ambalo alijinasiku kuwa linawezekana wakiingia ikulu. Aliongeza kuwa kipaumbele kingine ni Kilimo, ili kuweza kuleta ajira kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza zana za kisasa za kilimo na serikali kununua mazao kwa mkulima bila kuwakopa na endapo itakopa italazimika kulipa na riba. Aidha amelitaja suala zima la afya, ambapo alisema watajenga hospitali vijjini na kuakikisha kunakuwepo na huduma bora za upasuaji bila kutegemea kwenda katika mataifa mengine jambo ambalo limekuwa likiigharimu kiasi kikubwa cha fedha. Alisema kuwa ni lazima kuwe na mawasiliano thabiti ikiwa ni pamoja na kuifufua shirika la ndege la Tanzania kwani ni jambo la aibu kushindwa kuliendesha shirika hilo na kuliacha life. Alidai kinachotakiwa ni kulifanya shirika hilo kuwa la kibiashara zaidi. Lowassa amesema kuwa suala la maji hasa vijijini ni suala lililopewa kipaumbele kwani ndiyo wanawake wengi hutumia muda mrefu kutafuta maji na kusababisha kudorora kwa shughuli za maendeleo. Awali Mwenyekiti wa chama hicho Mbowe alisema mabadiliko hayatakuwa na maana kama hayataleta maendeleo kwa Watanzania, hivyo ni lazima maslahi ya raia yapewe kipaumbele, na waishi katika nyumba bora na siyo za tembe na kuwapa mwanga mpya wa maisha. Alisema kuwa wanachama waliokihama Chama Cha Mapinduzi wameleta chachu kubwa kwa UKAWA kwani umoja huo unatamani Watanzania kuondokana na umaskini na kuishi maisha bora zaidi. Aidha Mbowe amesema kuwa wao kama UKAWA wameridhika na Lowassa kwakua yeye ni chahcu ya maendeleo hana ubinafsi na si mnafiki na siku zote anapenda mabadiliko na kuongeza kua UKAWA watafanya kampeni safi zisizo na vurugu wala uvunjifu wa amani. Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye alisema kuwa CCM wameendesha siasa za chama kimoja kwa kujivika ngozi za vyama vingi na kuwataka kuwaacha watanzania kufanya maamuzi yao bila kuwazonga kwani wakati wa mabadiliko ni sasa na waache kuwajaza woga kuwa watakapo chagua upinzani wataaharibu nchi. Naye James Mbatia amewahakikishia Watanzaia wote wataishi katika maisha ya amani na maendeleo na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuachana na tabia ya uchochezi kwa taifa kwani watanzania ni wamoja na kufanya hivyo ni kuwagawanya na wao hawapo tayari kuona watanzania wakigawanyika. Mwenyekiti wa kamati ya uongoozi CUF, Waziri Msimo yeye amewapongeza Watanzania kwa kupokea mabadiliko yatakayo wapeleka kwenye maisha bora ya kweli na UKAWA ndio jibu lao la kweli. Naye Halima Mdee amewataka akina mama wote kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kwani akina mama ni jeshi kubwa na ndio watakao leta mabadiliko ya kweli ikizingatiwa wao ndio wanaotaabika katika kupata huduma bora za afya na kusababisha vifo vya kinamama na watoto wakati wa kujifungua, huduma za maji, elimu na uchumi duni na kusema kuwa wakati ni sasa kwani wanawake ni jeshi kubwa na wanatakiwa kufanya mabadiliko. Uzinduzi huo ulikuwa na kauli mbiu ya “LOWASSA MABADILIKO, MABADILIKO LOWASSA”.

UZINDUZI CHADEMA


Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa. Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward
Lowassa.[/caption]
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam Agosti 29, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika  Agosti 29, 2015. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika Agosti 29, 2015.
Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.
 PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...