|
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya (kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. |
|
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE inayotolewa na kampuni hiyo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akiwa katika mkutano huo. |
|
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya TTCL kuzinduwa teknolojia ya 4G LTE iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura. |
|
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya (kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. |
|
Uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE toka TTCL leo. |
|
Kulia ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE. |
|
|
Kulia ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE. |
|
|
Kushoto ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL na maofisa waandamizi wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE |
|
|
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imezinduwa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE unaoanza kutoa huduma jijini Dar es Salaam. Mtandao huo wenye teknolojia mpya na ya kisasa wenye kasi kubwa utatoa huduma katika maeneo 11 ambayo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere, Pugu Road, Posta Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay, Mwenge, Mbezi Tangibovu, Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala, na Wazi Tegeta.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizinduwa rasmi teknolojia hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema licha ya kuzinduwa huduma hiyo katika maeneo 11 kwa sasa mafundi wa kampuni hiyo wapo kazini wakiendelea na awamu ya pili ya kufunga mitambo ili huduma hiyo itolewe pia katika maeneo mengine 14 ya jiji la Dar es Salaam.
Aliyataja maeneo mengine ambayo mitambo inaendelea kufungwa kwa sasa kuwa ni pamoja na Kigamboni, Masaki, Temeke, Kimara, Jangwani, Kariakoo, Chuo Kikuu, Kurasini, Mbezi Chini Gongo la Mboto, Tabata, Kibamba, Kongowe na Bunju.
"...Awamu ya pili ya mradi huu itakuwa imekamilisha maeneo yaliyobaki ya mkoa wa Dar es Salaam na pia kupeleka mawasiliano hayo katika mikoa mingine ikiwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko," alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura.
Alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE unakuwa umekamilisha nia ya siku nyingi ya kampuni ya TTCL ya kuwahudumia wateja katika nyanja zote za mawasiliano (Fixed-mobile convergence) kwa kutumia teknolojia ya simu za mezani na simu za mkononi.
Akifafanua zaidi Dk. Kazaura alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuongeza kasi ya shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuchangia katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano na pia kuongeza uzalishaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.
Aidha aliongeza kuwa TTCL inaamini mtandao wa 4G LTE utafungua fursa pekee katika kukuza sekta ya elimu nchini kwa njia ya mtandao (E education). Na pia ubora wa huduma hiyo ya intaneti utatoa fursa kwa wanafunzi, wakufunzi, wataalam, wanazuoni na walimu kutumia teknolojia katika kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na nje ya taaluma.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akifafanua zaidi kwa wanahabari alisema mtandao wa 4G LTE utaongeza fursa katika sekta ya afya ambapo hospitali, vituo vya afya, vyuo vya afya na wadau mbalimbali wataweza kutumia mtandao huo katika kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi tena kwa haraka zaidi.
Alisema mtandao huo pia utazinufaisha sekta nyingine za kiuchumi kama vile sekta ya biashara, viwanda, kilimo na nyinginezo. "...Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wanahitaji mawasiliano ya uhakika katika shughuli zao. Mtandao huu wa 4G LTE utakuwa mkombozi wao na utaleta mageuzi katika kuongeza uzalishaji, kupanua wigo wa masoko ya bidhaa kwa wakulima, masoko kwa wajasiliamali, masoko kwa makampuni ndani na nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Peter Ngota.
Hata hivyo, Ngota aliongeza kuwa uzinduzi huo unaenda sambamba na uboreshaji vifurushi rafiki vya intaneti kwa wananchi hivyo kuwaomba wananchi kuiunga mkono kampuni ya kizalendo ya TTCL katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini.