Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.
























Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga akifungua mafunzo kwa wanahabari hawapo pichani yanayolenga kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya haki ya afya ya uzazi Changamoto wanazokutana nazo na namna ambavyo matumizi ya sheria za kimataifa kama Maputo Protocal yataweza kupunguza Chanagamoto hizo, Semina hiyo ya siku mbili ilikuwa ikifanyika Luther House Azania Front jijini Dar es salaam na imemalizika leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi ( wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho nkwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii(UDSM) Prof Godius Kahyarara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[/caption]
Na Raymond Mushumbusi ,MAELEZO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Dkt Abdallah Possi amezindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dkt Abdallah Possi amesema amefurahishwa sana kuona wasomi wa Tanzania wakijitolea muda wao na nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kuondokana na umasikini ili tuelekee katika ustawi wa taifa.
“ Kitabu hiki kimekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano imejikita katika mapinduzi na maendeleo katika sekta ya viwanda ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi nyingi duniani kwa sasa, hivyo tunaahidi kushirikiana na watafiti mbalimbali katika kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili katika kuondokana na umasikini,”Alisema Dkt. Possi.
“ Nimekisoma hiki kitabu kwa ufupi na kuona ni jinsi gani kitaweza kutusaidia katika mapambano dhidi ya umasikini lakini napenda kuwapa changamoto kuwa kazi hii ya kupambana na umasikini isiwe katika vitabu tu na sera bali iwe katika utekelezaji” Aliongeza Dkt Possi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akielezea jambo kwa washiriki na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli.[/caption]
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa watafiti wa mambo ya uchumi wanatakiwa kuwashirikisha pia watu wenye ulemavu katika harakati za kuondokana na umasikini kwa kuwashirikisha katika uundwaji wa sera na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya taifa.
Aidha Mhariri mkuu wa kitabu hicho, Prof Lucian Msambichaka amesema dhima kubwa ya kitabu hicho ni utekelzaji wa Sera,Mipango, Sheria na majukumu mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa taifa na kuongeza kuwa kitabu hicho pia kimetoa njia bora na muafaka wa kukuza sekta ya viwanda, kuboresha huduma za jamii, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na jinsi gani Tanzania inavyoweza kunufaika na maliasilia zake katika kujileta maendeleo.
Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kimeshirikisha waandishi zaidi ya 20 na kina kurasa zaidi ya 400 ambazo zimeelezea kwa kina namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kuondokana na umasikini na kuelekea katika ustawi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


