Saturday, August 19, 2017

NMB yazungumza na wajasiriamali Arusha Dodoma na Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christian Mndeme akizungumza alipokuwa akifungua warsha ya siku mojo ya Klabu ya wafanyabiashara wavBenki ya NMB Mkoa wa Dodoma iliyowajengea uwezo wa kibiashara wafanyabiashara.


Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghols akizungumza na wafanyabishara wa jiji la Arusha namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano na wajasiriamali toka Klabu ya Biashara ya NMB jijini humo.

Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya. 


Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya. 


Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya. 


Warsha ikiendelea.


Mgeni Rasimi kwenye Washa ya Klabu ya wafanyabiashara wadogowadogo na mawakala wa Benki ya NMB Mkoa wa Kilimanjaro, Sebastian Masanja Katibu tawala msaidizi toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mjini Moshi.



Mkurugenzi Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Tanzania Tom Borghols, akizungumza na washiriki wa Warsha ya Klabu ya wafanyabiashara wadowadogo na mawakala wa NMB Mkoa wa Kilimanjaro, warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kuringe Holl Mjini Moshi.


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola akitoa taarifa ya lengo la Benki ya NMB kuwakutanisha wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.

Baadhi ya wafanyabishara wa jiji la Arusha wakiwa katika mkutano huo.

UVCCM YALAANI UBAGUZI MISIKITINI PEMBA

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumzia kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)


Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)


Wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili  kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

UMOJA Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali ubaguzi uliofanywa na baadhi ya Wanachama wasikuwa CCM kwa kuwazuia wanachama wa CCM kuswali pomoja katika misikiti kwenye baadhi ya maeneo Mbalimbali visiwani Pemba.

Umoja huo umesema kuwa kuzuia watu kuswali kisa itikadi za dini zao ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani kufanya hivyo ni kupiga amri ya Mwenyezi Mungu anayetoa onyo Kali katika Quran kwa wale wanaothubutu kuwazuia waini wengine kuswali.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati alipotembelea Msikiti wa Masjid Lmuhajiriina uliopo Eneo la Kiungoni Kimango Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema kuwa Imani ya dini yoyote nchini haibagui wala kuchagua watu kuswali kutokana na Itikadi zao za kisiasa ama kikabila kwani dini Ni ibada ya Imani kwa kila mwananchi.

Shaka Alisema kuzuia watu kuabudu Ni makosa kwa mujibu wa taratibu za nchi lakini pia ni Dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani hakuna maandiko yanazuia watu kushiriki katika ibada.

Mnamo Mwaka Mwaka 2016 baada ya kura ya marejeo kikundo Cha watu wachache katika baadhi ya maeneo walianza kuwashawishi Wananchi kususia kuswali na Wanachama wanaotokana na CCM ambapo kwa kiasi kikubwa waliwaunga mkono Jambo lililopelekea waumini was kiislamu watokanao na CCM kuanza kusali majumbani mwao.

WANAVIJIJI IKUNGI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu (aliyesimama) amezindua awamu ya pili ya mradi wa kuwajengea wananchi uwezo ili kuibua na kuendeleza miradi ya maendeleo katika vijiji vyao wilayani humo.

Katika uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu alilipongeza shirika la HAPA kwa kusimamia vyema awamu ya kwanza ya mradi huo na hivyo kufanikisha kupata ufadhiri wa awamu ya pili ya mradi ambapo Vijiji 15 wilayani Ikungi vitanufaika.

Mhe.Mtaturu aliwata wasimamizi wa mradi huo kuendelea kusimamia vyema shughuli za mradi huo jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa miradi mingine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Ikungi.

Mkurugenzi wa shirika la HAPA, Makyao Noel alisema Vijiji 10 wilayni Ikungi vilifikiwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo na hivyo kusaidia wananchi kuibua miradi 26 ya maendeleo na kwamba miradi miradi 12 ilikuwa ya maji, Zahanati, Vituo vya Afya, barabara pamoja na nyumba za watumishi na kwamba awamu ya pili ya mradi huo itavifikia Vijiji 15 wilayani Ikungi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, akitoa neno la shukurani kwenye uzinduzi huo uliokwenda sambamba na kujadili mafanikio na changamoto za mradi wa awamu ya kwanza ili kusaidia uboreshaji kwenye utekelezaji wa mradi wa pili utakaodumu kwa miezi sita kuanzia mwezi huu.

Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.

Aliyesimama ni Mkurugenzi wa shirika la HAPA, Makyao Noel alisema, akitoa ufafanuzi kwenye uzinduzi huo.

Viongozi mbalimbali meza kuu.

Wawezeshaji wa mradi.

Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwemo madiwani wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo.

DC IKUNGI AZUNGUMZIA MICHUANO YA "IKUNGI ELIMU CUP"

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu ametoa ufafanuzi kuhusiana na ligi ya "Ikungi Elimu Cup 2017" itakayozinduliwa kesho Agosti 19,2017 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi wilayani humo.

Mhe.Mtaturu kaeleza sababu za kuanzishwa kwa ligi hiyo na namna itakavyosaidia kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika kutatua changamoto za elimu wilayani Ikungi ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara pamoja na nyumba za waalimu kupitia mfuko wa elimu Ikungi ambapo yeye ni mlezi wa mfuko huo.
BMG Habari

NEW SONG: Hear Our Cry - Varkeize Motema Feat. Larry SingLive and Daisy Nyokabi

This is a prayer for our beloved country Kenya and a call to all Kenyans to unite together. While many may have varied ways of championing for peace love and unity, this is my little contribution to this cause...

Below is youtube link to the video of the song.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...