Tuesday, May 2, 2017

VIDEO: KONGAMANO LA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA


Fuatilia yaliyojiri kwenye Kongamano la Wanataaluma na Wadau wa Habari kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, lililofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Kilele cha Maadhimisho hayo ni kesho Mei 03,2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
#BMGhabari

Miss Beatrice Enock wa EAGT Mwanza Alivyovishwa Pete ya Uchumba

Mtoto wa kiroho aliyezaliwa katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Mr.Peter Mlekwa, jana jumapili April 30,2017 amevisha pete ya uchumba, mchumba wake Miss Beatrice Enock pia wa kanisa hilo.

Zoezi hilo lilifanyika kanisani hapo chini ya Mchungaji Kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, ambapo wawili hao wapendanao walitambulishana mbele ya madhabahu katika kuianza safari yao ya ndoa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mr.Peter Mlekwa akimvalisha mchumba wake zawadi ya saa
Wachumba, Miss Beatrice Enock na Mr.Peter Mlekwa
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiwaombea wawili hao kuwa wachumba
Mchungaji Kulola (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachumba hao
Miss Beatrice Enock (kulia) akiwa na best lady wake, Happy Emmanuel
Muda wa pongezi kwa wachumba hao
Muda wa pongezi kwa wachumba hao
Muda wa pongezi kwa wachumba hao
Muda wa pongezi kwa wachumba hao
Waumini wa kanisa la EAGT Lumala Mpya katika picha ya pamoja na wachumba hao
Tunawatakia kila la Kheri katika Uchumba wao na katika kutimiza ndo yao ya kuifikia ndoa takatifu, Miss Beatrice Enock na Mr.Peter Mlekwa.

Harusi ya John Focus na Bi. Bernadetha Munishi Ilivyofana

 Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akimlisha keki mumewe John Focus Lyimo kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni.
Bwana harusi, John Focus Lyimo akimlisha ndafu mkewe kwenye hafla ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni kabla ya hafla hiyo.


Bwana harusi, John Focus Lyimo (katikati) akiandaa ndafu maalum kwa ajili ya kumlisha mkewe ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani mara baada ya ndoa yao. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi pamoja na wapambe wao wakiwa kwenye hafla hiyo.

  Bwana harusi, John Focus Lyimo (wa pili kushoto) akimtambulisha mkewe Bi. Bernadetha Munishi (wa pili kulia) kwa wageni waalikwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Waliokaa ni wapambe wa maharusi.


Dada na mashemeji wa bwana harusi...


Bwana harusi, John Focus Lyimo (kushoto) akipita meza hadi meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.


Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akipita meza kwa meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.

Maharusi wakiwaongoza wageni waalikwa kwenye maakuli...


Wanajumuiya wenzake na bwana harusi, John Focus Lyimo kutoka Temboni wakiongozwa na Mr&Mrs Msafiri wakishiriki katika hafla hiyo.

Kulia ni MC Leopold Sondoka (mwenye kipaza sauti) akitoa maelekezo kwa Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi kwenye hafla hiyo.

Wazazi wa Bwana harusi wakiongozwa na mwakilisha wa Baba ndg, Pius Elias (kushoto) wakizungumza machache kwenye hafla hiyo.

Wazazi na ndugu wa bibi harusi wakipata picha ya ukumbusho.

Familia ya bwana harusi ikiongozwa na mwakilisha wa baba ndugu, Pius Elias wakigonganisha glasi kwa furaha.


Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi wakionesha furaha yao kwa kugonga chiaz...

Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakigonga chiaz kwa furaha kubwa baada ya kufanikisha shughuli hiyo. Kutoka kushoto ni Mrs. Machonchoryo na Mrs Oscar Munishi.

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi wakiwalisha vipande vya ndafu 'mades' wao kama ishara ya kuwashukuru.

Wanakamati wakinyanyua keki waliopewa na maharusi kama shukrani kwa kujitoa na kufanikisha hafla hiyo..

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi (kushoto) wakimkabidhi keki ya asante Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia).

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia) akiwatambulisha wajumbe mbalimbali wa kamati yake.

Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...