Monday, August 29, 2016

Kampuni ya TTCL yamzawadia mwanariadha aliyeitoa Tanzania kimasomaso Olimpiki


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa kwanza kulia kulia) akimkabidhi tuzo mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. Wanaoshuhudia katikati ni baadhi ya wanariadha waliyoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (katikati) akizungumza kuwapongeza wachezaji hao. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) wakiwa katika hafla hiyo.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni kuwapongeza wachezaji wa timu ya Taifa Tanzania walioshiriki katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 yaliofanyika hivi karibuni jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Kampuni ya TTCL imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo. 

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Antony Mtaka akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliounda timu ta Taifa ya Tanzania kushiriki mashindano ya Olimpiki 2016 Rio.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Tuzo ya TTCL pamoja na zawadi kwa wanariadha walioshiriki mashindfano hayo ilikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Kulia ni baadhi ya maofisa wa TTCL wakiwa na tuzo hiyo.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.


Baadhi ya maofisa wawakilishi wa TTCL wakipiga picha ya pamoja na timu ya riadha iliyoiwakilisha Tanzania mashindano ya Olimpiki 2016 Rio, nchini Brazil.

Kampuni ya TTCL kusaidia mchezo wa riadha nchini KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) inafanya mazungumzo na vyama vya mchezo wa riadhaa nchini pamoja na wachezaji wa mchezo huo ili kuandaa mpango utakaowawezesha wanaridha kufanya mazoezi ya kutosha na hatimaye kufanya vizuri katika mashindano yao mbalimbali. Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo alipokuwa akitoa tuzo kwa mmoja wa wanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Mwanariadha Simbu alishika nafasi ya tano katika mbio za marathoni na kuvunja rekodi kwa wanariadha wa Tanzania. Kampuni ya TTCL mbali ya kutoa tuzo na fedha zitakazomsaidia mchezaji huyo akiwa mazoezini kwa sasa, imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo kutokata tamaa ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine yajayo. "...Kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura TTCL tumejiunga na wadau wengine wa michezo katika kuwapongeza wanamichezo wa timu ya Taifa ya Tanzania walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil, TTCL kwa nafasi yetu tumejiweka mstari wa mbele katika kuwasaidia wanamichezo wa riadha, tumejitolea kufanikisha timu ya riadha katika kukaa vizuri kimichezo..," alisema Mushi. "...Katika kipindi hiki cha michezo 2016 tumejitolea kuifanikisha timu ya riadha kuweza kushiriki vizuri katika programu za mazoezi, leo wakati wanarejea tumewaunga mkono kwa kutoa tuzo na fedha kwa msindi aliyefanya vizuri mwaka huu na pia kutoa fedha kwa wanamichezo wetu zitakazo wawezesha kufanya vizuri katika mazoezi yao, huu ni mwanzo lengo letu ni kwamba tutaweka utaratibu mzuri wa kuzungumza na vyama pamoja na taasisi zinazosimamia michezo hii ili kuona tunatengeneza utaratibu mzuri zaidi ambao ni endelevu utakaosaidia kukua kwa mchezo huu," alisisitiza meneja uhusiano huyo. Tuzo ya TTCL kwa Alphonce Simbu na fedha kwa wanariadha hao zilikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambapo aliwapongeza wanamichezo wote wa timu ya tanzania iliyokwenda nchini Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki 2016 kwa uzalendo waliouonesha kwa taifa licha ya changamoto anuai. Waziri Nnauye aliwaomba Watanzania kutowakejeli wanamichezo hao kwa maneno ya kuwakatisha tamaa na badala yake kuungana kuwapongeza na pia kutoa ushauri kwa wadau wa michezo ili Tanzania iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo, ikiwa ni pamoja na vyama vya michezo kusaidia kyuongeza idadi ya wachezaji wa timu ya Tanzania. Kampuni ya Multichoice Tanzania pia iliungana na TTCL na kuwazawadia ving'amuzi vya DSTV vilivyolipiwa kwa muda wa miezi sita wanamichezo wote wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016, pamoja na kumsaidia kumuwezesha mwanariadhaa Simbu programu za mazoezi kwa muda wa mwaka mmoja akiwa kama balozi wa kampuni hiyo. Timu ya Taifa ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 ilikuwa na wanamichezo saba, ambapo wanamichezo wanne walishiriki riadha, wawili waogeleaji na mmoja alishiriki mchezo wa judo.

Saturday, August 27, 2016

Kamati ya Bunge Tamisemi Yatembelea Mabasi ya Mwendo Kasi Dar

 Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart,  Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.

 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.

 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na  Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.

 Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.

 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.

  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.

Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.

Na Dotto Mwaibale

Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)

Simbachawene alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

"Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart" alisema Simbachawene.

Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.

Alisema changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.

Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni. 

Angalia Hafla ya Makabidhiano Uwanja wa Uhuru Dar...!


Friday, August 12, 2016

Mwenyekiti wa CCM, Dk Magufuli Awasili Jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).



Wizara ya Afya Wazungumzia Upungufu Chanjo ya Kichaa cha Mbwa na Homa Manjano

 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuagiza na kusambaza dozi mbalimbali za chanjo kupitia mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.

 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano na vitendo vya baadhi ya watumishi wa afya   wasiowaaminifu  ambao hulipwa fedha ili waweze kuwatengenezea wasafiri kadi za Chanjo ya Homa ya Manjano na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo kinyume cha sheria  na hatari kwa usalama wa Afya zao.

 Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dafrosa Lyimo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu zikiwemo za kifua Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambazo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.


Na Aron Msigwa, Dar es salaam

WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inatarajia kupokea dozi 14,000 za chanjo ya homa ya manjano mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2016 ili kutosheleza mahitaji ya wasafiri watakaohitaji huduma hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Aidha, Wizara hiyo imekwisha nunua dozi za chanjo ya Kifua Kikuu na Polio 739,700 na kusambaza dozi zipatazo milioni  7 kwenye mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed amesema kuwa uagizaji na usambazaji wa dozi hizo ni mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.

Akifafanua kuhusu kukosekana kwa baadhi ya chanjo ikiwemo ya Homa ya Manjano amesema hali hiyo imetokana na kutokea kwa mlipuko wa homa hiyo katika nchi za jirani ikiwemo Angola jambo lililosababisha akiba ya chanjo hiyo dunia nzima kupelekwa kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo kwa lengo la kuwachanja wananchi wote ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa.

Amesema kutokana na hali hiyo akiba iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kuzigawia nchi nyingine hasa matumizi kwa ajili ya wasafiri ilibidi ipelekwe katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa dozi hizo kutokana na uharaka na uhitaji wa chanjo hizo.

Amesema wizara kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) inatekeleza mradi wa majaribio wa kutokomeza kichaa cha mbwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar es salaam ambayo sasa ina chanjo za kichaa cha mbwa.

Amebainisha kuwa jijini Dar es salaam chanjo hizo zinapatikana katika hospitali ya wilaya ya Temeke, Kituo cha Afya Magomeni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watoto waliokosa chanjo katika awamu tofauti amesema kuwa wote waliokosa chanjo kuhakikisha kuwa wanamaliza chanjo zao kwa mujibu wa idadi ya chanjo walizopangiwa pindi zitakapopatikana.

Ametoa wito kwa wataalam wa afya wanaohusika na utoaji wa chanjo kuwapatia taarifa wazazi wenye watoto ambao walihudhuria vituo vya afya kisha kukosa chanjo hizo, kuhakikisha kuwa wanarudi katika vituo vya afya ili waweze kumalizia idadi ya chanjo walizotakiwa kupata pindi zitakapofikishwa kwenye vituo vyao.

 Kuhusu Mradi wa majaribio wa kipindi cha miaka 5 wa chanjo ya kichaa cha mbwa wenye lengo la kuondoa kichaa cha mbwa amesema kuwa unalenga kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo vya watu vinavyotokana na kichaa cha mbwa.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara hiyo Dk. Dafrosa Lyimo akifafanua kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo  zilizokuwa na upungufu hizo amesema kuwa mpaka sasa utaratibu wa kupokea chanjo zaidi  zikiwemo za kifua` Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambapo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.

Ametoa wito kwa wazazi wenye watoto waliokosa chanjo kuwasiliana na vituo husika ili waweze kupangiwa ratiba ya kupatiwa chanjo hizo kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali ndani ya umri wa miaka 5.





Waziri Nape alipozungumza na Wasambazaji wa Filamu na Muziki


Serikali yalifungia Gazeti la Mseto..!


SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...