Wednesday, July 27, 2016

Maalim Seif Kuhutubia Mkutano wa Uchaguzi Marekani

MAKAMO wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.

Maalim Seif Sharif Hamad  akiwasili katika uwanja wa ndege Philladelphia

Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwakhutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston.

Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja.

Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uiengerza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali. Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia.

Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Ukhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.

Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar.

Maalim Seif ambaye anafuatana na Mkuuwa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Bwana Issa Kheir Hussein, yupo nchini Marekani kuitikia mwaliko wa kuhudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democratic ulioanza jana jijini Philladelphia, mkutano ambao unatazamiwa kumpitisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa kuoitia tiketi ya Chama hicho.

Katika mkutano wake wa hadhara na Watanzania, Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, anatazamiwa kuzungumzia zoezi zima la uchaguzi huo uliofutwa, na kusisitza madai ya Chama chake ya kurejeshewa haki yao waliyoporwa katika uchaguzi huo, na mwenendo mzima wa Demokrasia nchini Tanzania.

Itafaa kukumbusha kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kuzuru Marekani katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Mwezi uliopita, Maalim Seif alikuwepo nchini humu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kisiasa na mashirika binafsi, na kutembelea Umoja wa Mataifa ambako alifikisha madai ya Chama chake ya ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania. Aidha alizungumza na Watanzania waishio nchini Marekani katika jiji la Washington.

Tuesday, July 19, 2016

Benki ya NMB yaorodhesha Hati Fungani zake kwenye soko la hisa, DSE



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (katikati) akipiga kengele kuashiria kuorosheshwa rasmi hati fungani za Benki ya NMB kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kulia).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Adelhelm Meru (katikati) akipiga makofi mara baada ya kuashiria kuorosheshwa rasmi hati fungani za Benki ya NMB kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 leo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kulia).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (Kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) mara baada ya tukio la Benki ya NMB kuoroshesha rasmi hati fungani kiasi cha shilingi bilioni 41.4 katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). 

  BENKI ya NMB leo imeorodhesha kiasi cha shilingi Bilioni 41.4 ilichokipata kutokana na mauzo ya hati fungani katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Tukio hilo limezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru kwa ishara ya kupiga kengele kwenye ofisi za DSM.

 Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Dk. Meru alipongeza hatua hiyo ya kuorodhesha hati fungani kwenye soko la hisa na kuongeza kuwa ni ya kizalendo na kuwataka wawekezaji katika sekta binafsi kushiriki kikamilifu.

 “Hati fungani hii inatarajiwa kuleta maendeleo katika soko la mitaji na inafungua njia kwa mashirika mengine binafsi, mashirika ya serikali na mamlaka za manispaa kutafuta njia mpya za kukuza mitaji na uwezeshaji” alisema Dk. Adelhelm.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NMB - Ineke Bussemaker alisema “Hati fungani hii ya miaka mitatu si tu imeleta msisimko chanya kwenye soko la mitaji bali hata katika soko la hisa, NMB inakuwa benki ya kwanza kupata Kiwango zaidi ya mara mbili ya Kiwango tulichoomba awali.” Bi Ineke.

Aliongeza kuwa mwitikio chanya kwenye hati fungani ya NMB unatoa somo kuwa kuna umuhimu wa benki mbalimbali kuchangia kwa Kiwango kikubwa katika kuendeleza masoko ya mitaji na pia kupigania elimu ya fedha kwa jamii. Hati fungani inayoorodheshwa leo ina riba ya asilimia 13 kwa mwaka na iitakomaa baada ya miaka miatatu. Bi Ineke alisema Kutolewa kwa hati fungani ya NMB ni sehemu ya mkakati wa benki kutafuta njia mbadala za vyanzo vya fedha.

Fedha zilizopatikana kwenye hati fungani zitatumika kwaajili ya kutoa mikopo kwa wateja, wateja watakaonufaika ni pamoja na wateja binafsi, wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na taasisi za serikali.

 Akiongea kwenye hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE - Moremi Marwa alisema “mafanikio ya Hati fungani ya NMB yanatuambia kuwa wawekezaji wanajua uwepo wa fursa zilizopo katika masoko ya mitaji na wana uwezo na hamu ya kusaidia wale walio na uhitaji wa kukuza mitaji yao.”

 Hati fungani ya NMB ilipata mwitikio chanya kutoka kwa wawekezaji na kupita Kiwango kilichopangwa awali kwa asilimia 107. Benki ilipata maombi 1,811 yenye thamani ya shilingi bilioni 41.4 huku maombi mengi yakirundikana wiki ya mwisho kabla ya kufunga upokeaji wa maombi.

Kutokana na kuorodheshwa kwenye soko la hisa, wawekezaji wataweza kuuza hati fungani zao kupitia soko la hisa la Dar es Salaam – DSE. Stanbic Bank Tanzania Ltd. Ndio wawezeshaji wa hati fungani ya NMB huku makampuni ya Orbit Securities Ltd. na EA Capital Ltd wakiwa kama mawakala viongozi.

Tuesday, July 5, 2016

BINTI WA MCHUNGAJI KULOLA APATA MWENZA.

Bwana Harusi, Richard Jeremiah Gwapulukwa (kushoto) wa Kasamwa mkoani Geita, amefunga ndoa na Happness Daniel Kulola (kulia) ambae ni binti wa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Ndoa imefungwa katika Kanisa hilo  na Mchungaji Paul Thomas Bagaka ambae pia ni msajili wa ndoa Manispaa ya Ilemela. Hafla ya ndoa hiyo inafanyika katika Ukumbi wa New Sun City Hotel Jijini Mwanza.


Maharusi wakiingia Kanisani kwa ajili ya Kufunga ndoa 
Maharusi wakisalimia. Pembeni ni wasimamizi
Mchungaji Paul Thomas Bagaka ambae pia ni msajili wa ndoa Manispaa ya Ilemela, akitoa somo la ndoa kabla ya kuwafungisha maharusi ndoa
Mchungaji Paul Thomas Bagaka awakiwafungisha maharusi ndoa
Bwana harusi akimvalisha bibi harusi pete ya ndoa
Bibi harusi akimvalisha bwana harusi pete ya ndoa
Maharusi wakiombewa na viongozi wa dini pamoja na wazazi
Maharusi pamoja na wasimamizi
Kutoka kulia ni Mchungaji  Dkt.Daniel Moses Kulola, Mama Mchungaji, Mercy Daniel Kulola, Mama mzazi na mchungaji na viongozi wa kanisa.
Brighters wakiingia ukumbini
Ndoa ilishuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
Na BMG


SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...