Tuesday, September 17, 2013

Severina Lwinga Ndiye Miss Personality 2013

Severina Lwinga afanikiwa kuingia katika fainali ya Miss Tanzania na kuungana na washiriki wengine na kukamilisha idadi ya watu watano mpaka sasa. Lwinga alilikwaa taji la Miss Personality baada ya kuwashinda warembo wenzake.
Mrembo Severina Lwinga juzi alifanikiwa kuwa mrembo wa tano kuingia nusu fainali ya shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 baada ya kutwaa taji la Miss Personality 2013. Mshindi wa taji hilo anapatikana kwa kupigigiwa kura na warembo wenzake.

Severina ameungana na Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo kuingia katika nusu fainali ya Miss Tanzania ambayo itafanyika Jumamosi hii ukumbi wa Mlimani City. Shindano hilo lilifanyika Mgahawa wa AK'S ulipo mtaa wa Samora.
 Warembo walioingia tano bora ya Miss Personality 2013 shindano lililofanyika katika magahawa wa AK'S uliopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Warembo watano ambao wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara jana. Kutoka kushoto  ni Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Personality, Severina Lwinga, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo.
Warembo wakiingia katika Mgahawa wa AK'S uliopo mtaa wa somora Dar es Salaam kushiriki shindano la Miss Personality.
 
 Warembo wakiwa ndani ya mgahawa wa AK'S jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akiwa na Mkurugenzi wa Mgahawa wa AK'S, Kishan.
 Warembo wakiwa eneo la juu la mgahawa huo ambako kuna patikana viywaji vya kila namna pamoja na burudani kali ya muziki.
Warembo wakiburudika kwa Disco safi lililopo ndani ya mgahawa huo wa Kimataifa wa AK'S.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...