Saturday, March 17, 2018

GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

 Wasamaria wema wakiwa wamewabeba watoto waliogongwa na gari la mizigo katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, eneo la Kituo Kipya, Gongo la Mboto, Dar es Salaam leo.

Na Richard Mwaikenda, GOMS

WATOTO wawili wamegongwa na gari la mizigo  katika ajali iliyotokea mchana wa leo 
katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, Gongo la Mboto (Goms), Dar es Salaam.

Watoto  hao wawili ndugu wa kike na wa kiume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka minne na mitano walipatwa na mkasa huo muda mfupi baada ya mama yao kuwaacha pembezoni mwa barabara.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema ajali hiyo ilitokea wakati gari  gari namba T 324 PTM lililokuwa kwenye mwendo kasi kuikwepa bodaboda iliyokuwa iliyokatiza ghafla mbele yake, ndipo likapoteza mwelekeo na kuwagonga watoto hao.

Gari hilo ambalo dereva alikimbia baada ya ajali kuogopa kipigo, liliwagonga watoto hao na kuingia kwenye mtaro, lakini kama siyo mtaro lingeingia kwenye nyumba na kusababisha maafa zaidi.Mwendesha bodaboda naye alikimbia kuogopa kipigo.

Watu wengine wakiwemo waendesha bodaboda wanaoegesha kusubiri abiria katika kona hiyo ilipo transfoma, walinusurika kwani wengi wao hawakuwepo na baadhi yao walikimbia baada kuliona gari hilo limekosa mwelekeo.

Wanasema kuwa mama mzazi wa watoto hao ambaye hakuwa mbali sana na eneo la ajali aposikia mkasa huo hakuamini na kilichofuata aliishiwa nguvu na kuanguka chini.

Baadhi ya wasamaria wema waliharakisha kuwachukua watoto hao waliokuwa kwenye hali mbaya na kuwaingiza kwenye Bajaji tayari kuwakimbiza hospitali kwa matibabu. 

Ajabu iliyotokea ni kwamba baadhi ya waendesha Bajaji walikataa katakata kuwapeleka watoto hao Hospitali.

 Watoto waliojeruhiwa wakiwa chini baada ya kuwaokoa chini ya gari kwenye mtaro

 Watoto majeruhi wakiingwa kwenye moja ya bajaji kuwawahisha hospitali, lakini hata hivyo mwendesha bajaji hiyo alikataa kuwapeleka na kuwaamuru wawashushe. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203,
 Wakihamia kwenye moja ya Bajaji kuomba msaada huo
 Wakiwaingiza kwenye Bajaji ambayo walikubaliwa
 Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akilia kwa uchungu baada ya kuwaona watoto hao
 Wakiangalia ajali hiyo
 Gari hilo nusura liingie kwenye maduka yaliyopo eneo hilo, kilichozuia ni mtaro wa maji taka,

 Trafiki akiangalia ajali hiyo

 Breakdown ikiandaliwa kulivuta gari. Hata hivyo lilishindwa
Gari hilo likivutwa na gari la taka

WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMANA KUTENGENEZA FURSA ZA KIUCHUMI


 Mkurugenzi wa Taasisi ya I-learn East Afrika, Noelah Bomani (Kulia) akimkabidhi tuzo Mwanamke aliyefanya vizuri na kuwa kivutio katika mafanikio yake katika kipindi cha mwaka 2017/2018, Joyce Ibengwe Nangai ambaye ni Meneja Mawasiliano na Masoko  wa Chama cha Waajiri  Tanzania (ATE). (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia mada.
Mawenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko akizungumza kuwaelezea  uzoefu aliopitia na kuwasisitizia umuhimu wa kuchangaman ili waweze kutengeza fursa za kiuchumi hata kijamii wakati wa usiku wa Wanawake na tunzo kwa Mwanamke aliyefanikiwa kwa mwaka 2018 iliyoandaliwa na Tasisi ya Shangwe ambapo wanawake kutoka sehemu mbalimbali walikutana na kuzungumza mambo ya ujasilimali na namna ya kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Meneja Bima ya magari kutoka shirika la Bima ya Taifa (NIC) Emakulata Mwaitege, akizungumza umuhimu wa Wanawake kujiwekea bima katika biashara zao na maisha yao hili waweze kusimama tena pindi majanga yanapowakuta.
Muigizaji na  Msanii waTabasam PR Consultant, Regina Beraldo Kihwele akitumbuiza  katika kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mshereheshaji wa Kongamano hilo, Angela Kileo akiwajibika katika hafla hiyo. 
 Meneja mafao kutoka mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Rosemary Mchagula akileza umuhimu wa wanawake kujiunga na mfuko huo kutokana na mafao yanayotolewa katika kuwasaidi kwa kulitaja fao la uzazi. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shangwe Event, Deus Ntukamanzina.
Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo  akichangia katika mada zilizokuwa zkitolewa kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifatilia matukio katika kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo  akichangia katika mada zilizokuwa zkitolewa kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. Kulia ni wazazi wa Afisa Mtendaji wa Shangwe Events, Deogratiasi Ntukamzina na Mke wake (wa pili kulia) 
Afisa Masoko wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Latifa Kigoda akileza ni namna gani wanawake wanaweza wakaungana na kuwa wawekezaji wakubw akatika mapinduzi haya ya uchumi wa Viwanda nchini.
 Mmoja ya Wanawake walioshiriki katika kongamano hilo kutoka TIB, Lisa Zavalla akichangia juu ya umuhimu wa wanawake kujikwamua kiuchumi katika mapinduzi ya uchumi wa Viwanda.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano hilo.
 Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano hilo. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Uchui na Uwekezaji Nchini (EPZA) Grace Lemunge . 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya I-learn East Afrika, Noela Bomani akieleza umuhimu wa wanawake kuchangamana na watu mbalimbali hili waweze kujikwamua kiuchumi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri fursa ziwafate.
Sehemu ya Wanawake waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mwanasaikolojia na Mshauri wa masuala ya familia, Sadaka Said, akieleza umuhimu wa mwanamke kuambatana na mabinti zao katika maisha hili kuwajenga kwa ajili ya kesho yao kuliko kuwaacha nyumbani.
Afisa Mtendaji mkuu wa Shangwe  Event, Deus Ntukamanzina akizungumza na  Wanawake waliofika katika hafla hiyo na kuwashukuru kwani kukutana kwao ndio mwanzo wa wao kupiga hatua kubwa zaidi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Secrets Lingerie, Fatna Tambwe (kushoto) na Afisa Masoko wa Kimtandao wa Mult-Choice Tanzania Grace Mgaya wakifuatilia mada katika konganano hilo. 

Mobile Week Kutoa Simu za Kisasa kwa Bei Che!

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott pamoja na Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto).

Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia, Zadok Prescott (wa pili kulia) 


akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). Waliombatana naye ni Mkurugenzi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohammed (wa kwanza kulia),  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto).

Mkurugenzi wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohammed (wa kwanza kulia)  

Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Simu (Mobile Week) itakayofanyika Machi 24 - 30 na kutoa ofa kabambe ya punguzo la bei kwa manunuzi simu za kisasa za mkononi kupitia tovuti ya Jumia (www.jumia.co.tz). 


WATEJA watafurahia punguzo kubwa la bei hadi 60% kwa simu za kisasa (smartphone) kupitia Jumia Mobile Week (wiki ya simu) itakayofanyika kwenye mtandao wa manunuzi ya bidhaa wa Jumia (www.jumia.co.tz). Pamoja na punguzo hili kubwa la bei, simu zote za kisasa zitakazouzwa katika promosheni hii zitakuwa na ofa ya hadi GB 18 ya intaneti bure kutoka kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania.

Katika uzinduzi wa gulio hilo la simu kwa njia ya mtandao, Jumia pia walizindua Ripoti ya Sekta ya Simu za Mkononi Tanzania inayoonesha kuwa asilimia 83% ya Watanzania walitembelea mtandao wa Jumia kupitia simu zao za mkononi, ikilinganishwa na asilimia 17% tu waliotumia kompyuta. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa Watanzania wengi wamevuka kigezo cha matumizi ya kompyuta na badala yake wanatumia teknologia ya  simu za mkononi kutekeleza shughuli zao za kila siku.

Akitangaza ushirikiano huo kabambe jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Mobile Week itakayoanza 24 – 30 Machi ndio muda muafaka zaidi wa kununua simu ya kisasa kwa sababu simu zote zitapatikana kwa bei nafuu zaidi ambazo hazijawahi kutokea nchini, huku kila simu ikiwa na ofa ya hadi GB 18 za intaneti kutoka Tigo.

‘Tigo inaongoza katika mageuzi ya maisha ya kidigitali. Lengo letu ni kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wote wanapata huduma bora, za uhakika za mtandao. Huduma bora za kidigitali zinaanza na vifaa  bora, ndio maana ushirikiano wetu na Jumia utahakikisha kuwa kila mmoja anapata simu mpya ya kisasa pamoja na ofa za intaneti zitakazomwezesha mtumiaji kuwa sehemu ya maisha ya kidigitali,’ alisema.

Akifafanua jinsi ya kupata ofa hizi za simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott aliwashauri wateja kutembelea tovuti ya www.jumia.co.tz ambapo watapata aina mbali mbali za simu kutoka kwa wauzaji mbali mbali. Baada ya hapo wanaweza kuchagua aina ya simu wanayoipenda na kutoa maelekezo ya sehemu ambapo wangependa kuletewa simu yenyewe na watoa huduma wa Jumia. Wasiokuwa na huduma za mtandao wanaweza kupiga simu namba 0800 710024 bila gharama yoyote ili kutoa maombi ya simu wanayoitaka.
‘Nawahamasisha nyote mchangamkie ofa kabambe za simu zitakazopatikana katika mtandao wa Jumia katika kipindi hiki cha Mobile Week. Tunafurahia kuleta pamoja baadhi ya kampuni kubwa zaidi za simu duniani kama vile Tigo,  Samsung, Tecno na Infinix kushiriki katika gulio hili la kila mwaka. Kwa pamoja tumefanikiwa kuwaletea ofa ambazo hazijawahi kutokea kwa simu za kisasa, ikiwemo simu zenye uwezo wa 3G zitakazopatikana kuanzia TZS 50,000/- pekee na zile za 4G zitakazopatikana kwa chini ya TZS 150,000/- tu,’ Zadok alisema.

‘Wateja wana uhuru wa kuja kuchukua simu zao kutoka katika ofisi za Jumia ama wanaweza kuletewa simu zao mahali popote walipo. Malipo kwa ajili ya simu yatafanyika kwa njia ya Tigo Pesa au kwa pesa taslim mara tu baada ya mteja kupokea simu aliyoagiza na sio vinginevyo. Hii inaondoa hofu ya  kutapeliwa,’ Zadok alimaliza.

Ukuaji wa simu za kisasa (smartphone) unatoa fursa kubwa kwa matumizi ya mtandao kutoa huduma mbali mbali kwa Watanzania kupitia mifumo kama Jumia. Hivi karibuni idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini ilifikia watu milioni 40, huku idadi ya wanaotumia mtandao ifikia watu 23 milioni.

“Idadi ya watu wanaotumia simu za kisasa inakua kwa kasi siku hadi siku. Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya simu za mkononi, ila upatikanaji wa vifaa vya kisasa bado ni changamoto kubwa. Jumia imejikita kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata simu za kisasa, hasa katika kipindi hiki cha Mobile Week,” Zadok alibainisha



Friday, March 16, 2018

Serikali yajipanga kupokea mradi wa Global Learning XPRIZE


  Serikali imesema inajiandaa kuupokea mradi wa ‘Global Learning XPRIZE’ unaowawezesha watoto walio nje ya mfumo rasmi kujifunza stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kupitia Michezo iliyowekwa kwenye tableti, kutoka kwa wadau wanaoufadhili baada ya kumalizika muda wa majaribio. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi akizungumza kuhusu maandalizi ya serikali kuupokea mradi wa Global Learning XPRIZE.
Kama serikali mradi unapomalizika tunaangalia namna ya kuuendeleza. Tutaendelea kushirikiana na halmashauri zetu zilizoko kwenye mradi wauone kama ni wa kwao na kwamba badala ya watoto kuzurura mitaani wanaendelea kujifunza,” amesema Mushi na kuongeza. “Tunaagiza wale wahusika, wadau wa elimu katika ngazi zote za kijiji hadi mkoa wa Tanga waone kama hiki kilicholetwa kwetu ni zawadi,na ni lazima kuuendeleza ili kupunguza watoto walioko nje ya mfumo rasmi; kwa maana hiyo inatakiwa tuwe na ushirikiano kuona changamoto baada ya huu mradi kumalizika ili kuzifanyia kazi.”
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.
Akielezea utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza na ulipofikia, Afisa Msaidizi wa Mradi kutoka UNESCO, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 2000 kutoka vitongoji 141 katika wilaya 6 za mkoa wa Tanga wamenufaika na mradi huo. “Baada ya miezi 15 ya mradi kukamilika, mradi utakabidhiwa kwa serikali ili kuendelea kuusimamia. , ambapo tumekutana leo Tarehe 13/3/2018 na wawakilishi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (BMT) , Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na TAMISEMI ili kuweza kuangalia ni jinsi gani watoto walio katika mradi wataingia katika mfumo rasmi katika ngazi husika,” amesema.
Wadau mbalimbali wakichangia katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

Washiriki wa mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...