Monday, April 4, 2016

SHIRIKA LA EfG LAFANYA TAMASHA LA KUPINGA UKATILI WA JINSIA

 Ofisa Ufutiliaji na Tathmini wa Shirika la Eguality for Growth (EfG), Shabani Lulimbeye, akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu vitendendo vya ukatili wa kijinsia katika Tamasha lililofanyika leo asubuhi viwanja vya Soko la Mchikichini Ilala jijini Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara katika soko hilo, Suleiman Azizi akichangia jambo kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi cha Temeke jijini Dar es Salaam kikihamasisha wananchi kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni katika Tamasha hilo.
 Wafanyabiashara ndogo ndogo katika soko hilo wakifuatilia tamasha hilo.
 Wasaidizi wa kisheria katika soko hilo wakiwa kwenye tamasha hilo. Kulia ni Zainab Namajojo na Mechi Mtindi.
 Wasanii wa kundi la Machozi wakila wakati wakiigiza igizo la kupinga ukatili wa kijinsia.
 Raia wa kigeni ambao wanafanyakazi ya kujitolea katika Shirika la EfG wakiwa kwenye tamasha hilo.
 Taswira katika tamasha hilo.
Wasanii wa Kundi la Machozi wakionesha igizo la ukatili wa jinsia masokoni.

TAASISI YA MANJANO WAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI DODOMA


Wanawake wa mji wa Dodoma walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani.




Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.
Awamu ya Saba na ya mwisho katika budget ya Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 150 kutoka mikoa Mitano Tanzania yamemalizika  Mkoani Dodoma. Wanawake 30 wa mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa wanawake hao 150 walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha na kuhitimisha na Mkoa wa Dodoma.
Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa na mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.


Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA

Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi huo.
Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Hoyce Temu
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (katikati) akiwa na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakikaribishwa ukumbini na kupewa kinywaji cha K -Vant ambao walikua wadhamini wa shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Lilian Kamazima
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 a-Hoyce Temu (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakifurahia kinywaji cha K-Vant.

Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkurugenzi wa Mwandago Investment, Chris Mwandago ambaye ni muandaji mashindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na kulia ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu.
 Fadhili Nkurlu
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akizungumza jambo.
Miss Tanzania Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akikata utepe kuzindua mashindano hayo jijini Arusha.  Miss Tanzania 1999  Hoyce Temu (kulia), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) na Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima.
Yamoto Band
Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Miss Tanzania Arusha 2016
Wadau wa tasnia ya urembo wakifurahia jambo.

HERI YA KUZALIWA KASINGE JOHNSON JUNIOR

Baba mzazi akimrisha keki birthday boy kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuzaliwa kwake huku mama akifurahia

 Mama mzazi wa birthday boy Kasinge Jr, Marian Johnson (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na birthday boy aliyetimiza mwaka 1 tokea kuzaliwa kwake na aunt pembeni

Madada wakifurahia

Watoto wakiendelea kucheza na kufurahia



Madada wakimlisha mdogo wao keki ikiwa ni ishara ya furaha ya kutimiza mwaka mmoja tokea kuzaliwa kwa mdogo wake


Sunday, April 3, 2016

HONGERA PATRICK MWAIPUNGU NA ROSEMARY RWECHUNGURA

SHEREHE YA KUTOA  POSA NA KUVALISHWA PETE YA UCHUMBA
BWANA HARUSI MTARAJIWA NDUGU PATRICK MWAIPUNGU NA BIBI HARUSI MTARAJIWA BI. ROSEMARY RWECHUNGURA NYUMBANI KWAO BI HARUSI MTARAJIWA  KWAMOROMBO JIJINI ARUSHA

Bw. Harusi mtarajiwa Patrick Mwaipungu akifurahi baada ya kumvisha pete mchumba wake Rosemary Rwechungura Kwamorombo Arusha. 


Wajomba wa Bw. harusi mtarajiwa ndg Patrick wakiwasili nyumbani kwa wakwe zao watarajiwa
Kwamorombo Arusha.


Mapokezi 


Ibada ikiendelea


Ndugu upande wa bwana harusi mtarajiwa


Bwana harusi mtarajiwa akiwa na mama yake mdogo wakifuatilia kwa karibu


Mshenga wa bwana harusi na ndugu wa bwana harusi Mwl Swai akizungumza na msemaji wa familia ya bibi harusi mtarajiwa Rosemary


Mshenga Mwl Swai akiweka mambo sawa na bwana harusi mtarajiwa


Baba na Mama wa bi harusi mtarajiwa Rwechungura


Mjomba wa bwana harusi Mtarajiwa ndg Denis akitoa utambulisho wa wageni waliofuatana nao.


Mshenga akikabidhi posa akisindikizwa na mjomba wa bwana harusi mtarajiwa.


Bi harusi mtarajiwa akikaribishwa ukumbini.

Bwana na bibi harusi watarajiwa


Bw. Patrick akikamilisha zoezi la pete

Bw. Patrick akimvisha Pete mchumba wake Rosemary.


Wakipongezana


Hongera sana

Wakipata chakula kilichoandaliwa kwa mapishi ya kabila la Wahaya



Mshenga akishukuru kwa zoezi zima kukamilika


MC Madam Happy akitoa shukrani kwa wageni waalikwa

Msemaji wa familia ya Mzee Rwechungura akitoa shukrani


DC SHINYANGA AMSWEKA RUMANDE MHANDISI WA MANISPAA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande Muhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada ya kupuuza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na Saruji kwa ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo kituo cha mabasi yaendayo wilayani.

Saturday, April 2, 2016

Serikali na TTCL kumiliki kwa pamoja Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiweka saini kitabu cha Wageni alipotembelea ofisi za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea ofisi hizo.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea ofisi hizo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TTCL Kigoma alipotembelea ofisi hizo. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni Meneja wa TTCL Kigoma, Bw Lugage Abdallah, Kaimu Mkuu wa Mkoa Kigoma, Bw Saveli Maketa, Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.


SERIKALI kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), zitamiliki kwa pamoja Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) ili kuongeza ufanisi wa mkongo huo katika kutoa huduma za mawasiliano nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema, Serikali ipo tayari kushirikiana na kampuni ya TTCL katika kuumiliki Mkongo huo kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na TTCL tangu mwaka 2010 ilipopewa jukumu la kuujenga, kuusimamia na kuuendesha Mkongo huo.

Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Simu TTCL Mkoa wa Kigoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 5 Mkoani humo kukagua shughuli za Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

Mhe Mbarawa alisema, Ombi lililotolewa na TTCL la kumiliki mkongo lina mantiki kubwa kutokana na uwezo wa kiufundi, kitaalamu na kiundeshaji uliopo ndani ya kampuni hiyo lakini kutokana na Sababu za kiserikali, ni lazima Serikali ibaki kuwa na mkono wake ndani ya Mkongo ili kuudhibiti, kuulinda kuhakikisha kuwa unatumika kwa tija na kufanya kazi zake kwa ufanisi.

"Tutaendelea kuzungumza Serikalini ili tukubaliane mgawanyo wa asilimia katika Mkongo wa NICTBB. Sina tatizo kuipa Ttcl asilimia hadi 70 na Serikali ibaki na asilimia 30. Cha msingi hapa ni kwamba lazima Mkono wa Serikali uwepo.. Huu ndio msimamo wangu kwa sasa, tutaendelea kujadiliana ili tuwe na namna bora zaidi ya kutekeleza mpango huu. Nia yangu na wenzangu wote Wizarani na Serikalini kwa ujumla, ni kuhakikisha Ttcl inaimarika na kuwa kinara katika huduma za Mawasiliano nchini" amesisitiza Mhe Mbarawa.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT, Wazalendo), Mhe Zito Kabwe alieongozana na Waziri Mbarawa katika ziara hiyo alisema, TTCL imeonesha uwezo mkubwa na jitihada za dhati tangu ujenzi hadi kuuendesha Mkongo kwa niaba ya Serikali na kushauri kuwa, wakati umefika kwa TTCL kukadhiwa mamlaka ya miundombinu hiyo ili kuipa TTCL nguvu zaidi na uhuru katika kuendesha chombo hicho.

"...Kwa maoni yangu, TTCL inastahili kukabidhiwa Mkongo wa NICTBB, wakipata mkongo huu wataimarika sana. Nimekuwa nikishauri mara zote kuwa, tukikabidhi Mkongo kwa TTCL tunaweza hata kuwapa jukumu moja tu la kufanya biashara ya Data, wakaachana na biashari nyingine ili waendeshe Mkongo kwa ufanisi" amesema Mhe Zito.

Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema, kampuni ya TTCL inaishukuru Serikali kwa nia njema ya kutaka kuimilikisha kampuni hiyo sehemu ya Mkongo kwa kuwa ni jambo lenye tija kibiashara na kuthamini juhudi kubwa na moyo wa uzalendo ulioneshwa na Wafanyakazi wa TTCL katika kuujenga na kuuhudumia Mkongo tangu kuanzishwa kwake.

Awali, Katika taarifa yake kwa Mhe Waziri, Meneja wa TTCL Mkoa wa Kigoma, Bw Lugage Abdallah alisema, Kampuni hiyo imejipanga kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma, kuongeza idadi ya Wateja na kutatua kwa haraka matatizo ya kiufundi yanapojitokeza ili kuwapa wateja huduma za uhakika.

"Mhe Waziri, tunakabiliwa na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Miundo mbinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Tunashirikiana na jamii na vyombo vya Ulinzi na Usalama kulinda miundo mbinu yetu na juhudi zimeanza kuzaa matunda kwa kukamata Wahalifu. Ombi letu kubwa kwako ni kuisaidia TTCL hasa katika kupata malipo ya huduma tunazotoa kwa Taasisi za Umma ambazo zimekuwa ni wadaiwa sugu" alisema Bw Abdallah.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amekamilisha ziara yake Mkoani Kigoma Jumamosi Aprili 02 na kuelekea Mkoani Katavi kwa ziara kama hiyo.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...