Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Monday, August 10, 2020

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad

Seif Shariff Hamad


KWA
mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amekiri hadharani kuwa amezeeka na kwamba yeye sasa ni Babu huku akimtaja Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa ni kijana mwenye nguvu. 

Akihutubia wafuasi wake katika Ofisi za ACT-Wazalendo, Vuga mara baada ya mapokezi ya wagombea wao, Seif Shariff Hama amesema “Pole Pole anasema kuwa mimi ni Babu, ati kizee! ni kweli nakubali kuwa mimi ni babu na wao mgombea wao  Dkt. Hussein ni kijana, sasa nataka kuwauliza wajukuu zangu leo mtanichagua mimi babu au kijana?” Aliwauliza wafuasi wake ambao wengi walibaki na midomo wazi. 

Mgombea huyo wa Urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, katika hali ya  kukata tamaa alieleza kuwa yeye akiwa Babu licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini atamshinda Mgombea Kijana wa CCM jambo ambalo liliwafanya wafuasi wake kuanza kuguna chini kwa chini huku akiwatuliza kwa kuwataka wasiwe na wasi wasi na uzee wake. 

Ifikapo Oktoba mwaka huu, Babu Seif Shariff Hamad atakuwa na umri wa miaka 78. Itakumbukwa kuwa Seif Shariff Hamad ni mgombea pekee aliyegombea mara nyingi  zaidi bila kushinda.

Alianza akiwa CCM Mwaka 1985 akashindwa na Sheikh Idriss –Abdulwakil, akaanza visa na vituko vya kuhujumu CCM ambapo Mwaka 1988 yeye na wenzake saba walifukuzwa Uanachama wa CCM. 

Mwana 1995 (uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi) aligombea na Dkt. Salmin Amour akashindwa. Mwaka 2000 aligombea na Amani Abeid Karume akashindwa. Mwaka 2005 aligombea tena na Karume akashindwa. Mwaka 2010 aligombea na Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Maalim Seif akaangukia pua.

Mwaka 2015 Maalim Seif aligombea tena na kushindwa. Mwaka 2020 anagombea na kijana Dkt. Hussein Mwinyi, na CCM wana uhakika wa  kumshinda 'asubuhi.' 

Hata mabango ya wafuasi wake pamoja na viongozi wenzake waliandika na kutamka maneno ya "Shikamoo Babu Seif"

Thursday, June 7, 2018

WAZIRI MKUU AWATAKA WABUNGE KUDUMISHA MSHIKAMANO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, baada ya futari aliyowaandalia, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasisitiza wabunge waendelee kudumisha  mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa nchi tulivu na yenye amani.

Amesema mshikamano na upendo walionao wabunge hao ni vema wakauendeleza ili waweze kutekeleza shughuli zao za kuishauri Serikali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo Juni 5, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma wakati wa futari aliyowaandalia wabunge. Futari hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa vyama vyote.

"Mshikamano na upendo huu tuliouonesha kuanzia mwanzo wa mkutano wa Bunge naomba tuudumishe ili tuweze kuishauri vizuri Serikali na tufikie malengo tuliyojiwekea,” alisema. 

Naye,Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye alitoa neno   la shukurani kwa niaba ya wabunge wote alimshukuru Waziri Mkuu kwa heshima aliyowapa.

"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii heshima uliyotupa ni kubwa, kualikwa na wewe si jambo dogo si kila mtu anaweza kupata nafasi hii," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mgogoni, Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf ambaye alisoma dua alisema watu wanatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliowapa.

“Kuna wenzetu tulioshirikiana nao kwenye mfungo wa Ramadhani mwaka uliopita lakini leo hatunao sababu wametangulia mbele ya haki, hivyo sisi tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupa,” alisisitiza.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...