BENKI ya NMB Tanzania imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Star Times ambapo kwa sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi. Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za Star Times, ambapo Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa alisema wateja wa NMB waliounganishwa na huduma za kibenki kwa simu za mkononi sasa watafanya malipo yao popote walipo na kwa urahisi, huku wateja wa Star Times ambao hawana akaunti na benki hiyo kuweza kulipia huduma katika tawi lolote la Benki ya NMB. Alisema huduma hiyo licha ya kuwarahisishia kazi wateja itakuwa haina tozo kwa wateja wa NMB hivyo kuwataka wananchi na wateja wa Benki ya NMB waitumie ipasavyo. Alisema hatua ya Benki ya NMB yenye zaidi ya wateja milioni mbili Tanzania huku ikiwa na matawi zaidi ya 176 itasogeza zaidi huduma za malipo ya ving'amuzi vya Star Times kwa wateja mbalimbali. Kwa upande wake Meneja Masoko wa NMB, Bwana Damien alisema wateja wa NMB na wengine wasio na akaunti watakapoitaji huduma ya malipo watatakiwa kubofya *150*66# na kuchagua huduma ya malipo ya Star Times na kuendelea kupata maelekezo rahisi katika kufanikisha malipo yao.
Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Wednesday, June 29, 2016
Wateja NMB Sasa Kupata Huduma za Vifurushi vya Star Times
BENKI ya NMB Tanzania imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Star Times ambapo kwa sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi. Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za Star Times, ambapo Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa alisema wateja wa NMB waliounganishwa na huduma za kibenki kwa simu za mkononi sasa watafanya malipo yao popote walipo na kwa urahisi, huku wateja wa Star Times ambao hawana akaunti na benki hiyo kuweza kulipia huduma katika tawi lolote la Benki ya NMB. Alisema huduma hiyo licha ya kuwarahisishia kazi wateja itakuwa haina tozo kwa wateja wa NMB hivyo kuwataka wananchi na wateja wa Benki ya NMB waitumie ipasavyo. Alisema hatua ya Benki ya NMB yenye zaidi ya wateja milioni mbili Tanzania huku ikiwa na matawi zaidi ya 176 itasogeza zaidi huduma za malipo ya ving'amuzi vya Star Times kwa wateja mbalimbali. Kwa upande wake Meneja Masoko wa NMB, Bwana Damien alisema wateja wa NMB na wengine wasio na akaunti watakapoitaji huduma ya malipo watatakiwa kubofya *150*66# na kuchagua huduma ya malipo ya Star Times na kuendelea kupata maelekezo rahisi katika kufanikisha malipo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...

-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Ilikuwa ni harusi ya kifahari; Aprili 29 itabaki kuwa siku ya kumbukumbu ya milele kwa wanandoa Prince William pamoja na mkewe Catherine (...
No comments:
Post a Comment