Wednesday, May 18, 2011

Ajali ya kutisha Geita, watu 15 wafa, 67 wajeruhiwa vibaya

Geita
WATU 15 wakiwemo watoto wawili, askari polisi mmoja wa jijini Mwanza wamepoteza maisha na wengine 67 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Sheraton lenye namba T 268 AJC na basi la Bunda Expres namba T 810 BDW baada ya kugongana uso kwa uso eneo la Kijiji cha Chibingo Wilaya ya Geita mkoani Mwanza.

Ajari hiyo ambayo imetokea jana mjini hapa majira ya saa tatu asubuhi eneo la barabara kuu ya Mwanza-Bukoba imehusisha mabasi mawili na roli la mizigo aina ya Fusso namba T 823 BDV baada ya basi la Sheraton lililokuwa likitoka Ushirombo Shinyanga kwenda Mwanza, kutaka kulipita lori lililokuwa likipanda kilima cha Chibingo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio wamesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa madereva wa mabasi hayo huku yule wa basi la Sheraton akitupiwa lawama kwa kushindwa kufuata sheria za barabarani kutokana na kutaka kulipita gali lililokuwa kwenye kilima bila kuhofia atari yoyote eneo hilo.

“Tulikuwa tukitokea Shinyanga kwenda Mwanza na basi la Sheraton tulipofika Kijiji cha Chibingo dereva wetu alijalibu kulipita gari la mizigo, lakini alishindwa kulimudu gari kisha kugongana uso kwa uso na basi la
Bunda hali iliyosababisha vifo...huu ni ukiukaji wa sheria za barabarani,” alisema, Yunusu Mathias.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita, Dk. Abdallah Dihenga amethibitisha kupokea miili 15 na majeruhi zaidi ya 60 na kuongeza kati yao watu sita wamepelekwa katika hospital ya rufaa ya Bugando Mwanza baada ya hali zao kuwa mbaya.

Alisema madaktari wanaendelea kuwahudumia majeruhi hao na hali zao zinaendelea vizuri baada ya wengine saba kutibiwa na kuruhusiwa, huku akiwataka ndugu, jamaa na marafiki kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kutambua  miili ya marehemu ambao wamehifadhiwa chumba cha maiti hospitalini hapo.  

Kutokana na ajali hiyo mamia ya wananchi wamefulika katika eneo la tukio wakisaidia kutoa miili ya marehemu na majeruhi katika magari yaliyo gongana uso kwa uso licha ya zoezi hilo kuwa gumu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutoklea huduma ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...